Bunge la Macao, China lapitisha mswada wa kuanzisha kamati ya kulinda usalama wa taifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2026
Bunge la Macao, China lapitisha mswada wa kuanzisha kamati ya kulinda usalama wa taifa
Bunge la Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao likifanya mkutano wa wajumbe wote wa kujadili na kupitisha mswada wa Kamati ya Kulinda Usalama wa Taifa ya Mkoa wa Utawala Maalumu wa Macao huko Macao, kusini mwa China, Machi 19, 2026. (Xinhua/Cheong Kam Ka)

MACAO - Bunge la Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao lilifanya mkutano wa wajumbe wote jana Alhamisi, ambapo limejadili na kupitisha mswada wa Kamati ya Kulinda Usalama wa Taifa ya Mkoa wa Utawala Maalumu wa Macao.

Chombo hicho cha kutunga sheria kimesema kuwa, ukiwa katika mfumo wa sheria, mswada huu umeweka bayana kuhusu kazi, muundo na mfumo wa utendaji kazi wa kamati hiyo, ili kamati hiyo iweze kutenda kazi kwa mujibu wa sheria thabiti zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha