Lugha Nyingine
Kenya yaanzisha ujenzi wa Reli ya SGR ya Naivasha-Kisumu-Malaba (3)
NAIROBI - Kenya imefanya hafla ya kuweka jiwe la msingi katika Kaunti ya kusini magharibi ya Narok jana Alhamisi, kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya SGR ya Naivasha-Kisumu-Malaba, mradi mkubwa wa miundombinu unaolenga kuhimiza mafungamano ya mawasiliano ya kikanda na ukuaji wa uchumi.
Mradi huo, utakaotekelezwa na Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China (CCCC), utajengwa kwa vipindi viwili. Katika kipindi cha 2B, njia ya reli itaunganisha Naivasha na Kisumu. Sehemu hiyo ya njia itakuwa na urefu wa kilomita takriban 264, ikihusisha njia ya tawi yenye urefu wa kilomita 8.9 hadi Bandari ya Kisumu. Na katika kipindi cha 2C ujenzi wa reli utaendelea kufanyika kutoka Kisumu hadi Malaba kwenye mpaka wa Kenya na Uganda, reli ambayo itapitia kaunti muhimu magharibi mwa Kenya.
Reli hiyo ni sehemu muhimu ya Ushoroba wa Kaskazini, ikiunganisha Kenya na nchi majirani zake zisizo na bahari, ikiwa ni pamoja na Uganda na Sudan Kusini, na inatarajiwa kuhimiza biashara na mafungamano ya kikanda.
Kwenye hafla hiyo, Rais wa Kenya William Ruto amesema, kuongeza urefu wa njia hiyo ya reli hadi mpaka wa Uganda kutasaidia kusukuma mbele mageuzi ya kijamii na kiuchumi kwa kupitia kuimarishwa kwa mawasiliano na ujumuishi wa kikanda.
"Leo inaashiria wakati mwingine tena muhimu katika mageuzi ya kiuchumi wa Jamhuri yetu," Ruto amesema, akieleza kuwa vipindi hivyo viwili vina nguvu bora kubwa, kwa kuunganisha jiji la bandari la Mombasa na maeneo ya ndani ya bara yenye utajiri wa maliasili ya kilimo, kupunguza gharama za usafirishaji, kuongeza kazi za kusafirisha bidhaa na kuchochea ongezeko la uchumi.
"Mradi huu pia utatoa nafasi za ajira na pia kuunga mkono kampuni katika wakati wa ujenzi wake kwa kupitia kuhimiza usambazaji wa bidhaa, biashara na kukuza vituo vya uzalishaji bidhaa," ameongeza.
Meneja mkuu wa CCCC Song Hailiang amesema kuwa reli hiyo ya SGR ni sehemu muhimu ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na mradi huo utahimiza ongezeko la uchumi wa Kenya wakati huohuo utaimarisha uhusiano wa pande mbili za China na Kenya.
"Mradi huu utafuata vigezo vya juu vya ubora na ufanisi, na kutoa kipaumbele kwanza kwa kutumia nguvu kazi za watu wa Kenya na kuhamisha teknolojia," Song ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




