Mabalozi wa nchi mbalimbali wapongeza maendeleo na ufunguaji mlango wa Mkoa wa Xinjiang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 23, 2026
Mabalozi wa nchi mbalimbali wapongeza maendeleo na ufunguaji mlango wa Mkoa wa Xinjiang, China
Martin Mpana, balozi wa Cameroon nchini China, akizungumza kwenye mkutano wa kubadilishana maoni mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 20, 2026. (Xinhua/Zhang Xiaoyu)

BEIJING - Wanadiplomasia kutoka nchi 40 na wajumbe wa mashirika ya kimataifa wamehudhuria mkutano wa kubadilishana maoni uliofanyika Beijing siku ya Ijumaa iliyopita, ambapo wamebadilishana maoni kuhusu maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii, hali inayoboreshwa siku hadi siku katika ulinzi wa haki za binadamu, na upanuzi wa ufunguaji mlango katika Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China.

Mario Alzugaray Rodriguez, konsuli wa ubalozi wa Cuba nchini China, aliyewahi kutembelea Xinjiang miaka 20 iliyopita, amesema kwamba mafanikio ya maendeleo ya Xinjiang tangu wakati huo ni ya kushangaza kweli, na amefurahia kufahamishwa kwamba Xinjiang sasa imekuwa na viwanja vya ndege zaidi ya 20, na mkoani humo kuna mtandao mpana wa reli na barabara kuu uliounganishwa vizuri.

Charymuhammet Shallyyev, mkurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kanda ya Asia ya Kati (CAREC), ameshuhudia maendeleo ya haraka ya mkoa huo. Amesema kuwa maendeleo ya Xinjiang yamewapa watu kumbukumbu nyingi za kuvutia hasa katika maeneo ya kutumia teknolojia ya AI, kufanya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na maendeleo ya kijani.

Takwimu muhimu za kiuchumi zilizotolewa kwenye mkutano huo zilipata kutambuliwa kwa wahudhuriaji mkutano. Takwimu hizo zinaonyesha kwamba mwaka 2025, pato la jumla la Xinjiang (GDP) lilifikia yuan trilioni 2.15 (dola za Marekani karibu bilioni 312.05), ambazo ni ongezeko la asilimia 5.5 kuliko mwaka 2024, na uzalishaji wa mafuta na gesi ulichukua nafasi ya kwanza nchini China kwa mwaka wa tano mfululizo.

Mwaka jana, wastani wa mapato ya kila mtu ya wakazi wake wa mijini na vijijini baada ya makato ya kodi uliongezeka kwa asilimia 5.3 na asilimia 7, mtawalia.

"Sikutegemea kwamba Xinjiang imekuwa na maendeleo ya kasi kubwa kiasi hiki," amesema Diane Sidikiba, konsuli wa uchumi na kaimu balozi wa Ubalozi wa Guinea nchini China.

Mabalozi wengine walioizungumzia Xinjiang kwa kuisifu wakiwemo pamoja na Balozi wa Pakistan nchini China Khalil-ur-Rahman Hashmi, Martin Mpana, balozi wa Cameroon nchini China, Selcuk Unal, balozi wa Uturuki nchini China, Sohail Khan, naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), Shakhrat Nuryshev, balozi wa Kazakhstan nchini China, na Charviakou Aliaksandr, na balozi wa Belarusi nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha