Lugha Nyingine
Kifaa cha kisasa cha kuchomelea chaanza kutumika kwennye eneo la ujenzi wa reli mkoani Zhejiang, China (6)
![]() |
| Mashine ya kuchomelea ya kutumia nishati mpya yanayotumika katika mazingira mbalimbali ikifanya kazi kwenye eneo la ujenzi wa Reli ya Mjini ya Hangzhou-Deqing, katika Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Machi 22, 2026. (Xinhua/Huang Zongzhi) |
Kwenye eneo la ujenzi wa Reli ya Mjini ya Hangzhou-Deqing, katika Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China mashine ya kuchomelea ya kutumia nishati mpya yanayotumika katika mazingira mbalimbali imeanza kutumika kwa mara ya kwanza kufanya shughuli za kuchomelea juu ya reli za chuma jana Jumapili.
Kifaa hicho kinatumia mfumo wa nishati mseto, kikiwa kimewekwa mfumo wa kisasa wa usimamizi wa nishati, na kinaunga mkono "kuchaji wakati wa kuchomelea." Kikichajiwa kikamilifu, kinaweza kukamilisha kwa kujitegemea kazi ya kuchomelea viunganishi 50 vya reli, na kwa hiyo kuhakikisha ujenzi tulivu unaoendelea katika maeneo yasiyo na vyanzo vingine vya umeme.
Reli hiyo, inayounganisha Eneo la Yuhang la Mji wa Hangzhou na Wilaya ya Deqing ya Mji wa Huzhou ikiwa na stesheni tisa kwenye njia yake, itaongeza zaidi mtandao wa usafiri wa reli wa Hangzhou itakapokamilika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




