Lugha Nyingine
Rais Xi ahimiza juhudi za kulijenga Eneo Jipya la Xiong'an kuwa kituo cha uvumbuzi, eneo la kielelezo cha maendeleo yenye sifa bora
XIONG'AN, Mkoa wa Hebei - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa wito wa juhudi za kulijenga Eneo Jipya la Xiong'an katika Mkoa wa Hebei kaskazini mwa China kuwa kituo cha uvumbuzi katika zama mpya na eneo la kielelezo cha kuhimiza maendeleo yenye sifa bora.
Rais Xi alikagua Eneo Jipya la Xiong'an jana Jumatatu, ambapo pia aliongoza kongamano juu ya kusukuma mbele zaidi ujenzi na maendeleo yenye sifa bora ya eneo hilo jipya.
Amesisitiza ni lazima kushikilia kwa uthabiti nafasi kuu ya jukumu la Eneo Jipya la Xiong'an la kuwa eneo muhimu la kubeba majukumu yasiyo ni lazima kubebwa na mji mkuu Beijing na yanayohamishwa huko.
"Eneo hili jipya linapaswa kuimarisha msukumo wake wa maendeleo kwa kupitia mageuzi na uvumbuzi, na kufungua nguvu hai kwa kupitia mkusanyiko unaofaa wa raslimali za uzalishaji na maliasili," Rais Xi amesema.
Siku ya Jumatatu asubuhi, Rais Xi aliwasili Xiong'an na kusafiri kwa gari kukagua maendeleo ya ujenzi katika sehemu ya kuanzisha kampuni mpya za uvumbuzi. Kisha alitembelea Kampuni ya Kundi la Huaneng la China, kampuni ambayo ilihamisha wafanyakazi zaidi ya 1,000 hadi Xiong'an Oktoba 2025, na alisikiliza ripoti kuhusu uhamaji wa kampuni hiyo, mpangilio wa viwanda na maendeleo ya uvumbuzi.
Akiwa kwenye kampuni hiyo, alikuwa na mazungumzo ya kikunjufu na wajumbe wa maofisa na wafanyakazi kutoka mashirika yaliyohama ambayo tayari yameanza kufanya shughuli zao katika eneo hilo jipya na yale yanayoendelea na ujenzi kwa sasa, ili kufahamu kuhusu maisha na kazi zao.
Rais Xi pia alitembelea kampasi ya Xiong'an ya Sekondari ya Juu ya Nne ya Beijing, ambapo alizungumza na walimu na wanafunzi darasani ili kufahamu kuhusu hali ya mafunzo huko. Kwenye kantini ya shule, alikagua mazingira ya kula na vyakula mbalimbali vilivyopikwa kantini.
Jumatatu alasiri, Rais Xi aliongoza kongamano hilo na kutoa hotuba muhimu. Amepongeza maendeleo muhimu yaliyopatikana katika ujenzi na ukuaji wa Eneo Jipya la Xiong'an. "Imethibitishwa vya kutosha uamuzi wa Kamati Kuu ya CPC wa kuendeleza eneo hili jipya ni sahihi kabisa, na kazi zote husika zimefanyika kwa hatua madhubuti na zenye ufanisi," ameongeza.
Rais Xi amesisitiza kufanya mpango wa jumla, na uratibu wa kuhimiza maendeleo yenye sifa bora na usimamizi wenye ufanisi wa juu, na kuhimiza kazi ya kukamilisha mfumo wa huduma za umma, kuhakikisha na kuboresha maisha ya watu, na kufanya juhudi za kutafiti namna ya kuwa na mifumo ya usimamizi wa mji wa kisasa unaoelekea siku za baadaye.
Rais Xi aliambatana na Waziri Mkuu wa China Li Qiang, mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC Cai Qi, na Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambao wote ni wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




