Lugha Nyingine
Tambi za mchele za Shengzha, ladha mpya ya urithi wa utamaduni usioshikika wa Guangxi, China (7)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 24, 2026
![]() |
| Watoto wakila tambi za mchele za Shengzha katika mashindano ya ufundi wa urithi wa utamaduni usioshikika katika Wilaya Inayojiendesha ya Kabila la Wayao la Dahua ya Mji wa Hechi, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Machi 21, 2026. (Xinhua/Huang Xiaobang) |
Tambi za mchele za Shengzha ni chakula kitamu cha jadi cha kienyeji katika Mkoa Guangxi, kusini mwa China kinachopendwa na wenyeji na watalii vile vile. Ufundi huo wa kutengeneza tambi hizi umeorodheshwa kwenye orodha ya urithi wa utamaduni usioshikika wa mkoa huo wa Guangxi.
Tambi za aina hiyo zinatengenezwa kwa viungo vya asili pekee na kwa kupitia mchakato wa kina ulio wa siku kadhaa za kuchagua mchele, kuchachusha mchele, kuusaga hadi kuwa unga, kukamua, kuchemsha kwa mvuke na kuukanda kuwa donge la unga. Hatua muhimu ni kuweka donge moja kwa moja kwenye maji yanayochemka ili kuunda kuwa tambi, halafu kuziopoa mara moja na kuweka viungo mbalimbali kwa kuandaliwa kuwa chakula kitamu cha tambi chenye ladha freshi kwa wateja.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




