Jukwaa la Wataalamu wa Mambo ya Fedha wa Nchi za Dunia ya Kusini 2026 lafanyika Beijing, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 26, 2026
Jukwaa la Wataalamu wa Mambo ya Fedha wa Nchi za Dunia ya Kusini 2026 lafanyika Beijing, China
Picha hii iliyopigwa Machi 25, 2026 ikionyesha hali ya Jukwaa la Wataalamu wa Mambo ya Fedha wa Nchi za Dunia ya Kusini 2026 mjini Beijing. (Xinhua/Zhang Shabiki)

BEIJING - Jukwaa la Wataalamu wa Mambo ya Fedha wa Nchi za Dunia ya Kusini 2026 limefunguliwa rasmi mjini Beijing jana Jumatano chini ya kaulimbiu ya "Kuangazia Nchi za Dunia ya Kusini" ambapo Mkuu wa Shirika la Habari la China, Xinhua Fu Hua alipohutubia jukwaa kuu alisema shirika la Xinhua limejitolea kupaza sauti ya Nchi za Dunia ya Kusini na kurekodi maendeleo yake yenye nguvu hai.

Ameongeza kuwa shirika hilo litatumia ipasavyo mtandao wake wa vyombo vyote vya habari na uwepo wake duniani kwa kuhimiza ushirikiano wa kina zaidi kati ya nchi za dunia ya kusini katika mambo ya fedha na kuchangia mpango wa utatuzi wa kujenga utaratibu mpya wa usimamizi wa mambo ya fedha duniani.

Sun Shuo, naibu meya wa Mji wa Beijing, amesema sekta ya mambo ya fedha ni nguzo ya uchumi wa Beijing. Amesema kuwa Beijing itaendelea kufungua mlango kwa kufuata vigezo vya juu na kupanua ushirikiano wa mambo ya fedha na Nchi za Dunia ya Kusini, kufanya juhudi za kuboresha mazingira ya biashara, kuimarisha mafungamano kati ya sayansi na teknolojia na mambo ya fedha, kusukuma mbele ushirikiano wa mambo ya fedha katika miradi ya kijani, na kuhimiza ufunguaji mlango wa kufuata vigezo vya juu zaidi katika mambo ya fedha.

Lu Lei, naibu mkuu wa Benki Kuu ya China, amesema benki kuu hiyo inazitia moyo taasisi za mambo ya fedha kufanya uwekezaji kwenye miradi ya kijani na inayotoa kaboni chache katika nchi na maeneo yanayoshiriki Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Ameongeza kuwa benki kuu hiyo inapenda kushirikiana na pande mbalimbali ili kusukuma mbele maendeleo yenye sifa bora ya mambo ya fedha katika miradi ya kijani na kuongoza mtaji kuelekea sekta za kijani na zenye kutoa kaboni chache.

Erwin Ramirez, waziri wa maendeleo, viwanda na biashara wa Nicaragua, na Shahin Mahmudzada, mkurugenzi mtendaji wa Benki Kuu ya Azerbaijan, pia walihutubia jukwaa hilo. Shughuli hii ya siku mbili imeandaliwa na Xinhua.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha