Maduro ajitokeza kwa mara ya pili katika mahakama ya New York (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2026
Maduro ajitokeza kwa mara ya pili katika mahakama ya New York
Waungaji mkono wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana nje ya mahakama, New York, Marekani, Machi 26, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

NEW YORK - Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amejitokeza kwa mara ya pili jana Alhamisi asubuhi katika mahakama ya New York baada ya kukamatwa kwake kwa nguvu na wanajeshi wa Marekani katika shambulizi la ghafla la kijeshi huko Caracas mapema Januari mwaka huu.

Wakati wa kushtakiwa kwake kwa mara ya kwanza Januari 5, Maduro alikana mashtaka yote ya Marekani dhidi yake, ikiwa ni pamoja na biashara ya dawa za kulevya, na aliiambia mahakama kwamba "alikamatwa kwa nguvu" kutoka kwenye nyumba yake ya kuishi ya Caracas, na yeye bado ni rais wa Venezuela.

Siku hiyo ya Alhamisi, katika mahakama, wakili wa Maduro aliendelea kumhimiza jaji kuondoa mashtaka hayo na akajenga hoja kwamba Marekani inazuia fedha za serikali ya Venezuela zisitumike kwa kulipa ada zake za wakili, na iko katika kuvamia haki ya Maduro kwa mujibu wa Katiba ya Nchi.

Ingawa ametilia shaka uhalali wa Washington kumzuia Maduro kutumia fedha za Venezuela kugharamia utetezi wake wa kisheria, jaji amekataa kufutwa kwa kesi hiyo. Januari 3, vikosi vya jeshi la Marekani vilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Venezuela na kumkamata kwa nguvu Maduro na mkewe, Cilia Flores, na kuwawasilisha hadi New York. Mashambulizi hayo ya Marekani yaliishtua jumuiya ya kimataifa, na kusababisha ulaumu na ufuatiliaji mkubwa duniani kote.

Wawili hao wamekuwa jela katika Kituo cha Kizuizi cha Metropolitan kilichoko Brooklyn, New York, tangu walipokamatwa huko Caracas.

Waandamanaji walikusanyika nje ya mahakama hiyo, ambayo ilikuwa katika ulinzi mkali wa watekelezaji sheria, wakipiga sauti na kutaka Maduro aachiliwe huru mara moja.

"Tuko hapa leo tukisimama na Nicholas Maduro na Cilia Flores," Jacoe Muldoon, mwandamanaji kijana, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua. "Tunadhani mashtaka yanapaswa kufutwa na wanapaswa kuachiliwa huru.

"Nchi nyingi zaidi zinapinga vitendo vya Marekani vya kujaribu kudumisha umwamba wake katika dunia," amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha