Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2026
Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
Picha iliyopigwa Machi 18, 2026 ikionyesha mandhari katika Eneo Jipya la Xiong'an, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China. (Xinhua/Yang Shiyao)

Tangu China ilipotangaza mpango wa kuanzisha Eneo Jipya la Xiong'an mwezi Aprili 2017, mji huo umeendelezwa na kubadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango. Kujenga Eneo hilo jipya kunalenga kupunguza kazi ambazo si za lazima kufanyika katika mji mkuu Beijing wa China na kusukuma mbele maendeleo ya eneo la Beijing-Tianjin-Hebei yaliyoratibiwa.

Katika miaka tisa iliyopita, mji huo wa Xiong'an, tangu mwanzo, umekuwa ukishikilia kufuata vigezo vya juu vya upangaji na usanifu, ukichukua mbinu ya "ujenzi wa miundombinu kwanza, kuingia kwa wakazi baadaye", likihakikisha ujenzi wa mitandao ya maji, umeme, gesi, barabara na madaraja inafanyika kwanza na kukamilika vizuri.

Ukiwa umepewa jina la "mji wa siku za baadaye," mji huo wa Xiong'an unapitia mabadiliko ya haraka. Takwimu rasmi zinaonyesha picha wazi zaidi: eneo lililoendelezwa limefikia ukubwa wa kilomita za mraba takriban 215 likiwa na majengo zaidi ya 5,300 yanayoonesha hali, sura na alama muhimu za mji, ambapo wakazi wamefikia milioni 1.41 na kampuni na viwanda vya teknolojia ya hali ya juu vimefikia 669.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha