Lugha Nyingine
ChinaVumbuzi | Ndege ya mizigo ya Changying-8 ya China inayojiendesha bila rubani yakamilisha usafiri wake wa kwanza (2)
ZHENGZHOU - Ndege ya mizigo ya Changying-8 ya China inayojiendesha bila rubani (UAV) imekamilisha usafiri wake wa kwanza kwenye uwanja wa ndege katika Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan, katikati mwa China jana Jumanne.
Ndege hiyo ya UAV yenye mabawa yasiyoweza kuhamishika au kupepea imeundwa na Kampuni ya Teknolojia ya Beifang Changying UAV ya Beijing, na ni jukwaa la kwanza la ndege ya mizigo ya UAV ya tani 7 nchini China iliyothibitishwa kupitia usafiri wa majaribio.
Ndege hiyo ya mizigo ya Changying-8 ya UAV ina sehemu kubwa ya mizigo yenye mita 18 za ujazo, uzito wa juu wa kupaa wa tani 7, na uwezo wa juu wa mzigo wa tani 3.5.
Inaweza kukidhi mahitaji mbalimbali ya upakiaji, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kawaida, bidhaa freshi na za mnyororo baridi, na zana za dharura. Ndege hiyo inajivunia uwezo wa kusafiri umbali mrefu zaidi wa kilomita zaidi ya 3,000.
Ndege hiyo ya mizigo ya UAV ina uwezo mpya katika usafirishaji wenye ufanisi wa juu, kuzoea hali mbalimbali kwa unyumbufu, na uwezo wa kusafiri kwenye maeneo ya aina zote, ikitoa uungaji mkono wa zana na vifaa kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa anga ya chini na ujenzi wa mifumo ya kukabiliana na hali ya dharura.
Inaweza kutumika katika kazi za kusafirisha bidhaa kwa masafa marefu, utoaji huduma ya uokoaji wa dharura, kutoa ugavi kwa eneo la mpakani, na uwezo wa uendeshaji kwenye mazingira ya hali ngumu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




