Lugha Nyingine
Milipuko kadhaa yasikika mjini Bujumbura, Burundi (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2026
![]() |
| Picha iliyopigwa Machi 31, 2026 ikionyesha moshi ukipaa angani baada ya milipuko kufuatia moto katika kambi ya kijeshi mkoani Bujumbura, Burundi. (Xinhua) |
BUJUMBURA - Milipuko kadhaa imesikika mjini Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi, jana Jumanne, wakazi waliliambia Shirika la Habari la China, Xinhua. Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii, na Usalama wa Umma ya Burundi imesema katika ujumbe kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii la X kwamba milipuko hiyo ilifuatia moto katika kambi ya kijeshi mkoani Bujumbura.
Jeshi la Ulinzi wa Taifa la Burundi limethibitisha kuwa milipuko hiyo ilitoka katika ghala la silaha kwenye Kambi ya kijeshi ya Bujumbura, ambako moto ulikuwa umezuka.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




