Lugha Nyingine
Viwanda vya teknolojia ya hali ya juu vya China vyarekodi ukuaji mkubwa katika robo ya kwanza ya mwaka
BEIJING - Takwimu za hivi punde za kodi zinaonyesha kuwa uchumi wa China umeendelea kuwa na utulivu, huku msukumo wa uvumbuzi ukiimarika, ikithibitishwa na ukuaji mkubwa wa mapato katika viwanda vya teknolojia ya hali ya juu katika robo ya kwanza ya mwaka 2026.
Takwimu hizo zilizotolewa Jumatano na Mamlaka ya Kodi ya China zinaonyesha kuwa mapato ya mauzo ya viwanda vya teknolojia ya hali ya juu kwa kipindi cha kuanzia Januari 1 hadi Machi 25 yaliongezeka kwa asilimia 14.6 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Viwanda na huduma za teknolojia ya hali ya juu vilishuhudia mapato yakikua kwa asilimia 12.7 na asilimia 15.8, mtawalia.
Yakichochewa na mahitaji ya AI na vituo vya nguvu ya hesabu, mapato ya mauzo ya usanifu na uzalishaji wa saketi jumuishi pia yalishuhudia ongezeko kubwa, takwimu hizo zinaonyesha.
Katika kipindi hicho, mapato ya mauzo ya sekta ya uzalishaji bidhaa yalikua kwa asilimia 5.4 wakati huohuo mapato ya mauzo katika nyanja za uzalishaji wa mashine na vifaa yaliongezeka kwa asilimia 6.3, takwimu hizo zinaonyesha.
Takwimu hizo za Jumatano pia zimedhihirisha kasi ya China katika mpito wa kijani, huku mapato ya mauzo ya sekta ya utunzaji wa ikolojia na mazingira asilia yakiongezeka kwa asilimia 9.6 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Mapato ya mauzo ya uzalishaji wa nishati safi yaliongezeka kwa kasi, yakichukua asilimia 36.3 ya jumla ya mapato yote ya mauzo ya uzalishaji wa umeme, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.5 ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita, takwimu hizo zinaonyesha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



