Lugha Nyingine
Afrika Kusini yazindua mkutano wa 6 wa uwekezaji ili kuvutia wawekezaji duniani

Mkutano wa sita wa Uwekezaji wa Afrika Kusini ukifanyika Johannesburg, Afrika Kusini, Machi 31, 2026. (Xinhua/Chen Wei)
JOHANNESBURG – Mkutano wa sita wa Uwekezaji wa Afrika Kusini umefunguliwa Jumanne wiki hii kwenye Kituo cha Mikutano cha Sandton jijini Johannesburg, ukiwaleta pamoja wajumbe zaidi ya 1,000 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 50 ili kuchunguza fursa za uwekezaji.
Akihutubia tukio hilo, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema mkutano huo unatoa jukwaa la kuonyesha nguvu za uwekezaji za nchi hiyo na kuunganisha wawekezaji na fursa halisi.
Akibainisha kuwa hali ya kutokuwa na uhakika kwenye uchumi duniani inaendelea kutokana na mivutano ya Mashariki ya Kati, amesema Afrika Kusini inatoa "pendekezo zuri ikiwa mahali pa uwekezaji penye uhimilivu, kuaminika na penye mwelekeo wa mageuzi."
Mkutano huo unafanyika chini ya mfumokazi wa "D tatu" -- kuondoa kaboni (decarbonization), mambo ya kidijitali (digitization), na uchumi wa sekta mbalimbali (diversification) -- huku uboreshaji wa urahisi wa kufanya biashara ukiwa kipaumbele mtambuka, rais huyo amesema.
Rais Ramaphosa amesema mikutano mitano ya kwanza ya aina hiyo, iliyofanyika kati ya mwaka 2018 na 2023, ilipata uwekezaji uliothibitishwa wenye thamani ya randi trilioni 1.5 (dola za Marekani karibu 88.4), ikizidi lengo la randi trilioni 1.
"Sisi ni nchi iliyo katika jitihada za mageuzi. Tunaweka mazingira kwa ajili ya ukuaji unaoongozwa na uwekezaji, ukuaji ambao ni mpana, jumuishi, na wa kudumu," ameongeza.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye Mkutano wa sita wa Uwekezaji wa Afrika Kusini, Johannesburg, Afrika Kusini, Machi 31, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Mkutano wa sita wa Uwekezaji wa Afrika Kusini ukifanyika Johannesburg, Afrika Kusini, Machi 31, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Wajumbe wakihudhuria Mkutano wa sita wa Uwekezaji wa Afrika Kusini, Johannesburg, Afrika Kusini, Machi 31, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye Mkutano wa sita wa Uwekezaji wa Afrika Kusini, Johannesburg, Afrika Kusini, Machi 31, 2026. (Xinhua/Chen Wei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



