Sera ya kutotoza ushuru ya China yachochea ukuaji wa viwanda nchini Ghana na bara la Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 02, 2026

Samuel Nii-Noi Ashong, mshauri mwandamizi wa sera katika usimamizi wa mambo ya fedha katika Wizara ya Fedha ya Ghana akizungumza wakati wa mazungumzo ya siku moja kati ya China na Afrika kuhusu sera ya kutotoza ushuru ya China, Accra, Ghana, Machi 31, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Samuel Nii-Noi Ashong, mshauri mwandamizi wa sera katika usimamizi wa mambo ya fedha katika Wizara ya Fedha ya Ghana akizungumza wakati wa mazungumzo ya siku moja kati ya China na Afrika kuhusu sera ya kutotoza ushuru ya China, Accra, Ghana, Machi 31, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Washiriki kwenye mazungumzo nchini Ghana wamesifu sera ya kutotoza ushuru ya China kwa Afrika, wakiielezea kuwa ni njia kuu ya kuendeleza mipango ya kiuchumi na ukuaji wa sekta ya viwanda ya kitaifa na bara zima.

Samuel Nii-Noi Ashong, mshauri mwandamizi wa sera katika usimamizi wa mambo ya fedha katika Wizara ya Fedha ya Ghana, ameielezea hatua hiyo kuwa ni "ya kipekee na ya kihistoria," akiihimiza Ghana kuitumia kikamilifu ili kuifanyia mageuzi sekta yake ya viwanda na kupata nafasi bora zaidi ya kibiashara na China katika siku zijazo.

Alitoa kauli hayo wakati wa mazungumzo ya siku moja yaliyofanyika chini ya kaulimbiu ya "Sera ya China ya kutotoza ushuru kwa Afrika: Fursa kwa Ghana" yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Urafiki kati ya Ghana na China na kufanyika Jumanne mjini Accra.

Kwa mujibu wa Ashong, utaratibu wa kutotoza ushuru hutoa manufaa ya moja kwa moja kwa sera ya uchumi wa saa 24 ya Ghana iliyozinduliwa hivi karibuni.

"Kwa mbinu na hatua sahihi za serikali, Ghana inaweza kutumia kikamilifu fursa hizi na kujenga uwezo mkubwa wa ushindani wa mauzo ya nje," amesema.

"Kuunganisha hatua hizi za ushuru na ujenzi wa uwezo unaolenga teknolojia, ikiwemo uhamishaji wa maarifa, kukuza mauzo ya nje kwa njia mahsusi, na kuanzisha ofisi maalum za biashara nchini China, kutasaidia kukuza bidhaa zinazotengenezwa Ghana moja kwa moja katika soko lenye watumiaji bilioni 1.4 nchini China," amesisitiza.

Katika mazungumzo hayo, Li Yaohong, mshauri wa uchumi na biashara katika Ubalozi wa China nchini Ghana, amesema kuwa sera hiyo ya ushuru inalenga kuchochea maendeleo ya viwanda na maendeleo ya jumla kote barani Afrika.

Amesema kuwa chini ya mfumo huo mpya wa upendeleo, majukwaa kama vile Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China na Maonyesho ya Canton hayatakuwa tu majukwaa ya kuonyesha bidhaa bali pia madaraja muhimu kwa kampuni za Ghana kuunganisha na wanunuzi wa China, kujenga utambuzi wa chapa, na kujumuika kwenye mnyororo wa thamani wa viwanda duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha