Lugha Nyingine
Tanzania yaongeza vikomo vya bei ya mafuta kutokana na kuvurugika kwa usambazaji duniani
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini Tanzania (EWURA) imetangaza bei mpya za kikomo kwa bidhaa za petroli huku kukiwa na kuvurugika kwa usambazaji duniani kunakotokana na siasa za kijiografia katika eneo la Mashariki ya Kati.
Katika taarifa iliyotolewa jana Jumatano na mamlaka hiyo, mabadiliko hayo ya bei ya mafuta kwa mwezi wa Aprili yametokana kwa kiasi kikubwa na mapigano yanayoendelea yanayohusisha Marekani, Israel, na Iran, ambayo yalianza mwishoni mwa mwezi Februari.
Chini ya bei hizo mpya za kikomo zilizoanza kutumika kuanzia Aprili 1, petroli jijini Dar es Salaam itauzwa kwa dola za Marekani takriban 1.53 kwa lita, huku dizeli na mafuta ya taa vikigharimu dola takriban 1.52 na 1.47 kwa lita, mtawalia.
Mamlaka hiyo imesema Tanzania inatekeleza hatua ili kuhakikisha usalama wa usambazaji wa mafuta huku ikipunguza athari za kiuchumi na kijamii, na imewasihi watumiaji kutumia mafuta kwa ufanisi wakati wa kipindi hiki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



