Lugha Nyingine
Watu 13 wafariki baada ya ghala la risasi kulipuka nchini Burundi
(CRI Online) April 02, 2026
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi wa Taifa la Burundi (FDNB) Bw. Gaspard Baratuza amesema, watu 13 wamefariki na wengine 57 kujeruhiwa, wakiwemo wanajeshi watatu, baada ya ghala la silaha katika kambi ya kijeshi iliyoko Bujumbura kulipuka Jumanne jioni.
Akizungumza na wanahabari jana Jumatano, Baratuza amesema, mlipuko huo ulisababishwa na moto uliozuka katika ghala la risasi la brigedi ya ugavi iliyoko katika eneo la Musaga wilayani Mugere. Amesema moto huo umesababisha uharibifu wa mali kwenye nyumba, magari binafsi, vifaa vya kijeshi na mitambo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



