Afrika Kusini yakaribisha uwekezaji wa China ili kuhimiza maendeleo ya uchumi

(CRI Online) April 02, 2026

(Xinhua/Chen Wei)

(Xinhua/Chen Wei)

Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushindani wa Afrika Kusini Bw. Parks Tau amesema Afrika Kusini inakaribisha ahadi za uwekezaji kutoka kampuni za China.

Akijibu maswali ya vyombo vya habari siku ya Jumanne kwenye Mkutano wa sita wa uwekezaji wa Afrika Kusini (SAIC) mjini Johannesburg, Bw. Tau amesema Afrika Kusini inatarajia "uhusiano imara zaidi wa uwekezaji na China."

Ameongeza kuwa uwekezaji wa China utasaidia mchakato wa maendeleo ya viwanda wa Afrika Kusini, na kutoa mchango kwa maendeleo ya uchumi.

Amesema Afrika Kusini imekuwa ikiwasiliana na China kwa ajili ya kuhitimisha mipango ya mavuno ya mapema chini ya Mfumo wa Makubaliano juu ya Ushirikiano wa Kiuchumi kwa Maendeleo ya Pamoja, mapema iwezekanavyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha