Lugha Nyingine
StanChart yazindua tena suluhusu za ushoroba wa biashara kati ya China na Kenya kwa kampuni ndogo na za kati
Benki ya Standard Chartered imezindua tena suluhusu za ushoroba wa biashara kati ya China na Kenya jana Jumatano ili kuimarisha kazi ya kampuni zenye ukubwa mdogo na wa kati (SMEs) katika biashara ya pande mbili.
Hatua hiyo inaziwezesha kampuni hizo za SME kwa kuzipa upatikanaji wa fedha ulioboreshwa, kupunguza gharama za miamala, na kuunganishwa moja kwa moja na masoko ya China, huku ikijikita katika sekta kama za uzalishaji bidhaa na nishati ya kijani.
Kiongozi wa kundi la China katika Benki hiyo Richard Li amesema hatua hiyo imepangiliwa ili kuwezesha wajasiriamali wadogo wanaofanya biashara kati ya China na Afrika kuweza kutumia sarafu mbalimbali katika kupata ufadhili wa kuaminika wakati wakikabiliana na mazingira magumu ya usimamizi.
Naye mkuu wa kitengo cha SME katika Benki ya Standard Charted Kenya, Bernard Kombo, amesema ushoroba wa biashara wa China na Kenya unatoa manufaa kwa SMEs kwa kuwa unatumia mfumo wa kimataifa wa malipo unaoweza kukamilisha miamala kati ya China na Afrika ndani ya sekunde 15 ikilinganishwa na njia za jadi ambazo zinachukua hadi siku mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



