“Feri ya Kikapu” ya Chongqing, China Yaipata Feri Mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 03, 2026

Qin Dayi akitazama nyuma kumtazama “rafiki yake wa zamani” feri ya “Yuzhongke 2180” baada ya kumaliza kuisafisha, Machi 30, 2026. (Picha na Xinhua)

Qin Dayi akitazama nyuma kumtazama “rafiki yake wa zamani” feri ya “Yuzhongke 2180” baada ya kumaliza kuisafisha, Machi 30, 2026. (Picha na Xinhua)

Asubuhi ya Machi 31, katika gati la Yangdu, Wilaya ya Zhongxian, Mjini Chongqing, feri ya zamani na mpya ya “Yuzhongke 2180” zilikuwa zimetia nanga sambamba, zikiwa zimetulia kwenye mwambao.

Kapteni Qin Dayi alikuwa akizunguka hapa na pale kwenye feri ya zamani kwa muda mrefu, akifanya ukaguzi wa kina kila mahali, kabla ya kuchukua kitambaa na kufuta kwa makini mabenchi ya mbao. Mabenchi hayo yamekuwa yakiambatana naye, mshirika wake Cao Lifang, na wakulima wenyeji wa mboga za majani kupita miaka 14. Leo hii, feri hiyo ya zamani itakamilisha jukumu lake, na feri mpya, pana na yenye mwangaza wa ndani, iko tayari kuchukua nafasi yake.

Feri ya zamani na mpya ya “Yuzhongke 2180” zikiwa zimetia nanga sambamba kwenye gati. (Picha na People’s Daily)

Feri ya zamani na mpya ya “Yuzhongke 2180” zikiwa zimetia nanga sambamba kwenye gati. (Picha na People’s Daily)

“Kapteni Qin, usiwe mzito kuliacha lipite. Mara utakapoanza kusafiri kwenye feri mpya, itakuwa rahisi zaidi kwako,” mkulima mmoja alimwambia Qin, akimwita apande feri hiyo mpya.

“Hiyo ni kweli, itakuwa rahisi na bora zaidi kwa nyie abiria pia- safi na joto zaidi,” Qin Dayi alimjibu, huku akichukua kikapu kizito cha mkulima huyo na kukiweka kwa makini kwenye deki ya feri.

Simulizi hiyo ya “Yuzhongke 2180” ilianza mwaka 2012. Mwaka huo, Qin na wanakijiji wenzake walishirikiana kununua feri hiyo ya abiria, ikitoa huduma kati ya Wilaya ndogo ya Yangdu na Wilaya ya Zhongxian. Kila asubuhi, ilikuwa ikitoka Yangdu, kupitia gati tisa kando ya mto, ikihudumia wakulima wa eneo hilo.

Kwa wakulima hawa, ingawa mabasi ya abiria yanatoa huduma ya haraka, ni ghali zaidi, na yasingeweza kubeba kilo nyingi za mboga za majani zisizokunjwa au ndege hai. Kwa maana hiyo, “Feri hii ya kikapu” inaendelea kuwa chombo muhimu cha usafirishaji kwao.

Hata hivyo, juhudi za kuiweka feri hiyo katika huduma zimezidi kuwa ngumu. Katika miaka 10 iliyopita, bei za tiketi hazikuwahi kupanda; wastani wa yuan 5 (takriban shilingi 1880 za Tanzania) kwa safari moja, na yuan 12 (takriban shilingi 4500 za Tanzania) kwa safari ya kwenda na kurudi, wakati gharama ya mafuta kwa safari hiyo moja pekee ni karibu yuan 600 (takriban shilingi 225800 za Tanzania), ikisababisha kujiendesha kwa hasara kwa muda mrefu.

Mwaka 2022, Qin alifikiria kuuza feri hiyo mara moja. Kabla ya kuiuza, aliipiga picha za mnato na video na kuziweka mtandaoni. Bila kutarajia, video hizo zikavuma. “Hii imenikumbusha wazazi wangu” na “Inachochochea kupakumbuka nyumbani,” watumiaji wa mtandao walijaza maoni kwenye ujumbe wake huo, na kutuma vidokezo vya pesa. Ingawa hali hiyo ilipunguza shinikizo la kifedha, uzee wa feri na hatari za usalama vilibaki.

Tangu mwaka 2025, Kituo cha Mambo ya Baharini cha Chongqing kimekuwa kikihimiza mpango wa uboreshaji wa hali ya usalama kwa feri za abiria za vijijini, kikianzisha mfumo wa ruzuku wa mnyororo mzima ili kutatua changamoto zinazowakabili wamiliki; “kusita kuziboreshaau ukosefu wa fedha.”

Feri hiyo mpya ya “Yuzhongke 2180” ni ya kisasa, ina urefu wa mita 38.5 na upana wa mita 6.4. Deki iliyopanuliwa inaongeza nafasi ya kuhifadhi mazao ya kilimo, ikiwa na nafasi zaidi kwa wakulima kuweka vikapu vyao. Ikiwa imesanifiwa kuendeshwa kwa kasi ya km 17.5 kwa saa, feri hiyo inajivunia ukinzani wa upepo ulioboreshwa sana, na imewekwa vifaa kamili vya kiyoyozi, mfumo wa kuzalisha umeme kwa jua, na vya kuhifadhi taka.

Feri mpya ya “Yuzhongke 2180” ikiwa imebeba matunda na mboga freshi za majani kwenye Gati la San Tiao Ling, Wilaya ya Zhongxian, Machi 31. (Picha na Zheng Yu, Chongqing Daily)

Feri mpya ya “Yuzhongke 2180” ikiwa imebeba matunda na mboga freshi za majani kwenye Gati la San Tiao Ling, Wilaya ya Zhongxian, Machi 31. (Picha na Zheng Yu, Chongqing Daily)

Cao Lifang (kulia) akiendesha feri mpya ya “Yuzhongke 2180”, huku Qin Dayi akitoa tahadhari ya kuwa makini, Machi 31. (Picha na Zhao Jun, People’s Daily)

Cao Lifang (kulia) akiendesha feri mpya ya “Yuzhongke 2180”, huku Qin Dayi akitoa tahadhari ya kuwa makini, Machi 31. (Picha na Zhao Jun, People’s Daily)

Baada ya simulizi hiyo ya feri mpya ya “Yuzhongke 2180” kujulikana sana, mamilioni ya watumiaji wa mtandao walijiunga na matangazo ya moja kwa moja mtandaoni, wakapanda feri hiyo binafsi, kununua mboga za majani, na watu wa kujitolea walitoka sehemu mbalimbali kusaidia kusafirisha na kuuza mazao. Feri hii ndogo si tu inabeba mboga za majani, bali pia wema dhahiri miongoni mwa watu.

Sasa, feri hiyo mpya inaendelea kwa usalama na abiria. Ndani ya sehemu ya kukaa abiria, matangazo ya moja kwa moja ya simu yanaendelea kurekodi maisha ya kila siku ya feri. Kwa uungaji mkono wa sera na ulinzi wa nia njema, “njia hii ya kikapu” ya majini inaendeshwa kwa utulivu.

Safari ya kwanza ya feri mpya ya “Yuzhongke 2180” ikikaribia kituo cha mwisho kwenye gati ya Xishan, Machi 31. (Picha na Zheng Yu, Chongqing Daily)

Safari ya kwanza ya feri mpya ya “Yuzhongke 2180” ikikaribia kituo cha mwisho kwenye gati ya Xishan, Machi 31. (Picha na Zheng Yu, Chongqing Daily)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha