Katibu Mkuu wa UN atoa wito kwa mara nyingine tena kuzitaka Marekani na Israel kukomesha vita dhidi ya Iran

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 03, 2026

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Aprili 2, 2026. (Xinhua/Xie E)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Aprili 2, 2026. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres ametoa wito wake kwa mara nyingine tena kuzitaka Marekani na Israel kukomesha vita dhidi ya Iran, na kuitaka Iran kuacha kushambulia majirani zake.

"Maana ya wito wangu ni wazi. Kwa Marekani na Israel, ni wakati muafaka wa kukomesha vita vinavyosababisha mateso makubwa kwa binadamu na kusababisha matokeo kama balaa katika mambo ya uchumi. Kwa Iran, pia ni wakati wake wa kuacha kushambulia majirani zake," katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema jana Alhamisi kwenye hotuba kwa waandishi wa habari.

"Mgogoro wa Mashariki ya Kati umeingia katika mwezi wake wa pili, na uharibifu wake mkubwa, mashambulizi yasiyotofautisha hali, na mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia yanazidi kupamba moto bila kusita, " amesema.

Guterres amedhihirisha kuwa mgogoro huo umeleta athari kwa sehemu mbalimbali duniani, ameonya kwamba dunia iko kwenye ukingo wa vita vikubwa zaidi ambavyo vitaikumba Mashariki ya Kati nzima na kuleta athari kubwa kote duniani.

Amesema juhudi za kidiplomasia zinaendelea ili kupata njia ya amani ya kusonga mbele, ambayo "inastahiki kupata nafasi na uungaji mkono ili kufanikiwa kutokana na sheria za kimataifa, pamoja na Katiba ya Umoja wa Mataifa."

"Migogoro lazima itatuliwe kwa njia ya amani. Mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi wa Nchi Wanachama wote lazima viheshimiwe. Raia na miundombinu ya kiraia, ikiwemo majengo ya nyuklia, lazima viheshimiwe na kulindwa. Na uhuru wa usafiri lazima uhakikishwe ," amesema.

"Lazima tupate njia ya amani ya kumaliza migogoro," katibu mkuu huyo amesema, akiongeza kuwa "migogoro haijiishii yenyewe. Na wakati viongozi wanapochagua mazungumzo badala ya uharibifu, ndipo migogoro inapoweza kukomeshwa." 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Aprili 2, 2026. (Xinhua/Xie E)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Aprili 2, 2026. (Xinhua/Xie E)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha