Lugha Nyingine
Rwanda yapata mkopo wa IMF wa dola za kimarekani milioni 250 kuunga mkono mageuzi ya kiuchumi na utulivu
(CRI Online) April 03, 2026
Wizara ya Fedha na Mipango ya Kiuchumi ya Rwanda imetangaza kufikia makubaliano na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuhusu mpango wa mkopo wa miezi 38.
Wizara hiyo imetoa taarifa jana Alhamisi ikisema, makubaliano hayo yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 250 yatawasilishwa kwa viongozi wa IMF na Bodi yake ya Utendaji kwa idhini ya mwisho, inayotarajiwa Juni 2026.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makubaliano hayo yataiunga mkono Rwanda kuendeleza mageuzi, kusimamia uchumi, kujenga tena kinga za kifedha, na kukabiliana na athari za vita katika Mashariki ya Kati.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



