Lugha Nyingine
Idadi ya watalii wa kigeni wanaowasili Kenya yaongezeka kwa asilimia 9 mwaka 2025
Sekta ya utalii nchini Kenya imerekodi ukuaji imara mwaka 2025, huku watalii wa kigeni wanaowasili nchini humo ikiongezeka kwa asilimia 9.
Ripoti iliyotolewa na Wizara ya Utalii na Wanyamapori ya nchini humo jana Alhamisi imesema, sekta hiyo, ikichochewa na sera ya kufutwa kwa visa na kuongezeka kwa safari za ndege, imerekodi ukuaji endelevu mwaka 2025, na kuthibitisha tena nafasi yake ya kimkakati ya kuwa msingi muhimu wa uchumi wa taifa.
Ripoti hiyo imesema, sekta ya utalii imeingiza shilingi trilioni 0.5 kwa mapato ya jumla, na kuakisi uimarikaji endelevu, unyumbufu na maboresho ya utendaji.
Wizara hiyo imesema, ukuaji huo pia unaakisi nafasi ya kimkakati ya Kenya ndani ya nyanja ya utalii duniani, hususan kutokana na ushindani wa vivutio vya utalii kwa ajili ya nafasi ya kupanua soko la kimataifa la usafiri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



