Lugha Nyingine
Watu wanane waliofukuzwa kutoka Marekani wawasili nchini Uganda
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uganda Bw. Simon Mundeyi amesema, watu wanane waliofukuzwa kutoka Marekani wamewasili nchini Uganda, na kuzua mjadala mpya kuhusu mchango wa nchi hiyo katika kupokea raia wa nchi ya upande wa tatu.
Katika taarifa yake ya Alhamisi Bw. Mundeyi amesema, watu hao, wanaume saba na mwanamke mmoja kutoka Mauritania, Angola, Ethiopia, Mali, Togo na Guinea waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, na wameandikishwa kama watafutaji wa hifadhi.
Mwezi Agosti mwaka jana, Uganda ilisema imefikia makubaliano na Marekani kupokea raia wa nchi ya upande wa tatu ambao wanashindwa kufikia vigezo vya hifadhi nchini Marekani, lakini hawataki au hawawezi kurudi katika nchi zao za asili.
Serikali ya Uganda imesema, nchi hiyo itaweka kipaumbele kwa watu kutoka nchi za Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



