Lugha Nyingine
China yaripoti kuongezeka kwa matumizi wakati wa mapumziko ya Siku ya Qingming
BEIJING – Takwimu zilizotolewa na idara za serikali ya China zimeonesha kuwa matumizi wakati wa siku tatu za mapumziko ya Siku ya Qingming yameongezeka, ambapo mapumziko hayo kwa watu yalikutana na mapumziko ya majira ya mchipuko kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika sehemu mbalimbali nchini humu, hivyo limetokea wimbi la usafiri wa watu.
Wakati wa siku hizo za mapumziko kuanzia Aprili 4 hadi 6, wastani wa mauzo ya siku ya rejareja na ya migahawa yaliyofuatiliwa na Wizara ya Biashara ya China uliongezeka kwa asilimia 2.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa, matumizi ya malazi ya hotelini kwenye majukwaa makubwa yaliongezeka kwa asilimia 2.6 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho, wakati huohuo usafiri wa watu katika miji mbalimbali nchini umeongezeka kwa asilimia 15.1.
Katika siku hizo za mapumziko kwa watu, oda za kukodisha magari ziliongezeka kwa asilimia takribani 40 kuliko mwaka uliopita, zikichochewa na ongezeko la usafiri wa watu wa familia moja moja, wizara hiyo imeeleza.
Takwimu hizo za wizara pia zinaonyesha kuwa wakati wa siku hizo za mapumziko kwa watu, mapato ya mauzo mtandaoni ya bidhaa za teknolojia ya AI zikiwemo miwani, saa, kifaa cha kupima sukari kwenye damu, yamepata ongezeko kubwa.
Tarehe 5 Aprili mwaka huu ni Siku ya Qingming, au Siku ya Kufagia Makaburi. Hii ni siku ya jadi ya China kwa watu kutoa heshima kwa watu waliofariki dunia na kuabudu mababu zao. Siku hiyo ya jadi imewapa watu siku chache za mapumziko kwa kushiriki katika shughuli za nje na utalii wa kutazama mandhari.
Inakadiriwa kuwa usafiri wa abiria umefikia mara milioni 845.38 kote China wakati wa siku hizo za mapumziko, na ni ongezeko la asilimia 6 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana. Wastani wa usafiri wa watu kwa siku ulifikia mara milioni 281.79, mamlaka za usafiri za China zimesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



