Vyama vya upinzani na raia wa Japan waandamana kupinga hatua ya serikali ya kulegeza vizuizi vya usafirishaji wa silaha nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2026

Watu wakishiriki kwenye maandamano nje ya kituo cha Ikebukuro, Tokyo, Japan, Aprili 5, 2026. (Xinhua/Li Ziyue)

Watu wakishiriki kwenye maandamano nje ya kituo cha Ikebukuro, Tokyo, Japan, Aprili 5, 2026. (Xinhua/Li Ziyue)

TOKYO – Viongozi waandamizi kutoka vyama kadhaa vya upinzani vya Japan walijiunga na maelfu ya raia nje ya kituo cha Ikebukuro chenye watu wengi mjini Tokyo Jumapili jioni kupinga msukumo wa serikali unaoonekana kuwa hatari wa kulegeza vizuizi vya usafirishaji wa silaha nje na kusukuma mbele upanuzi mkubwa wa kijeshi, wakielezea wasiwasi kuhusu mwelekeo wa siku za baadaye wa nchi hiyo.

Watu zaidi ya 6,000 walihudhuria maandamano hayo, kwa mujibu wa waandaaji. Waandamanaji walishikilia mabango yaliyoandikwa "Nguvu ya jeshi haiwezi kuleta amani" na "Takaichi jiuzulu," huku wakipaza kaulimbiu ikiwemo "Pinga vita" na "Linda amani," katika kupinga kile walichokielezea kuwa ni mabadiliko katika sera ya usalama ya serikali.

Vyombo vya habari vya Japan viliripoti hapo awali kwamba serikali ya Waziri Mkuu Sanae Takaichi inapanga kurekebisha miongozo ya utekelezaji wa "kanuni tatu za uhamishaji wa vifaa na teknolojia ya ulinzi" ndani ya mwezi huu ili kulegeza vizuizi vya usafirishaji wa silaha nje.

Watu wakishiriki kwenye maandamano nje ya kituo cha Ikebukuro, Tokyo, Japan, Aprili 5, 2026. (Xinhua/Li Ziyue)

Watu wakishiriki kwenye maandamano nje ya kituo cha Ikebukuro, Tokyo, Japan, Aprili 5, 2026. (Xinhua/Li Ziyue)

Wanasiasa wa upinzani waliokuwa wakizungumza kwenye mkutano huo walisema kuwa usafirishaji wa silaha wa Japan nje ya nchi unaweza kuchochea migogoro ya kimataifa na unapingana na kanuni za amani zilizowekwa kwenye katiba ya nchi hiyo.

Wameonya kwamba mfululizo wa sera zinazosukumwa na serikali, zikiwemo kuimarishwa kwa kijeshi kusikokoma, sheria inayopendekezwa ya kupambana na ujasusi, na mipango ya kuanzisha shirika la kitaifa la ujasusi, zinaweza kuiweka Japan katika njia hatari kuelekea kujiandaa kwa vita.

Tomoko Tamura, mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha Japan, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano kwamba katiba ya Japan inakataza waziwazi nchi hiyo kuanzisha vita, kutatua migogoro ya kimataifa kwa nguvu, au kushiriki katika migogoro ya kimataifa.

"Iwe ni kusafirisha silaha nje au kumiliki makombora yenye uwezo wa kushambulia nchi nyingine, hatua hizi lazima zipingwe vikali. Lazima tuzuie juhudi za kuigeuza Japan kuwa 'taifa linalopigana vita,'" amesema.

Tetsu Tatara, mwakilishi wa waandaaji wa mkutano huo, ameliambia Xinhua kwamba msukumo wa utawala wa Takaichi kwa upanuzi mkubwa wa kijeshi na usafirishaji wa silaha nje unasimama "kinyume na matakwa ya umma."

Watu wakishiriki kwenye maandamano nje ya kituo cha Ikebukuro, Tokyo, Japan, Aprili 5, 2026. (Xinhua/Li Ziyue)

Watu wakishiriki kwenye maandamano nje ya kituo cha Ikebukuro, Tokyo, Japan, Aprili 5, 2026. (Xinhua/Li Ziyue)

Amesema hatua za serikali za kuimarisha uwezo wa kijeshi na kuweka makombora, zikitumia kile kinachoitwa "tishio la China" kama kisingizio, zimezua wasiwasi mkubwa nchini Japan, na kusababisha idadi inayoongezeka ya raia kupaza sauti za upinzani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha