Rais Xi ampongeza To Lam kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Vietnam

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2026

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa salamu za pongezi jana Jumanne kwa To Lam kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Vietnam.

Rais Xi akisema kuwa China na Vietnam ni jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ambayo ina umuhimu wa kimkakati, amesema katika miaka ya hivi karibuni, chini ya uelekezaji na uhimizaji wa pamoja wa viongozi wa vyama na nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Vietnam umepata maendeleo makubwa, na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote umetoa matokeo mazuri, na kuleta manufaa halisi kwa watu wa nchi zote mbili.

"Tangu mwanzo wa mwaka huu, pande hizo mbili zimedumisha mawasiliano ya kimkakati kwenye ngazi ya juu na kusukuma mbele hatua kwa hatua ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote, zikionyesha vya kutosha urafiki mkubwa wa makomredi na ndugu," amesema.

Rais Xi amesisitiza kwamba, katika kukabiliana na mabadiliko ya kasi ambayo hayajapata kushuhudiwa katika miaka mia moja iliyopita, mshikamano na uratibu wa karibu zaidi kati ya China na Vietnam unalingana na maslahi ya pamoja ya vyama na nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema kwamba anaweka umuhimu mkubwa kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya vyama viwili na nchi hizo mbili, na anapenda kushirikiana na To Lam katika kusukuma mbele maendeleo na ustawishaji wa kitaifa, kuhimiza maendeleo ya hatua madhubuti ya ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja, kuimarisha siku hadi siku mambo ya kijamaa ya kila upande, na kunufaisha vizuri watu wa pande hizo mbili, ili kuingiza utulivu mkubwa zaidi na nguvu za kuhimiza juhudi katika kanda na dunia.

Pia siku hiyo ya Jumanne, Waziri Mkuu wa China Li Qiang alimtumia Le Minh Hung salamu za pongezi kwa kuchaguliwa kwake kuwa waziri mkuu wa Vietnam.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha