Lugha Nyingine
Hatua za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hazipaswi kutoa uhalali wa matumizi ya nguvu: Mjumbe wa China
UMOJA WA MATAIFA – Hatua za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hazipaswi kutoa uhalali wa matumizi ya nguvu, sembuse kuongeza mvutano na kuchochea zaidi hali hiyo, amesema Fu Cong, mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, jana Jumanne.
Baraza la Usalama limeshindwa kupitisha mswada wa azimio ambalo "linahimiza sana" nchi zenye nia ya kutumia njia za kibiashara za usafirishaji wa baharini kwenye Mlango Bahari wa Hormuz kuratibu juhudi zenye muundo wa kujilinda ili kusaidia katika kuhakikisha usalama wa usafiri wa meli katika mlango-bahari huo, ikiwemo kwa kusindikiza meli za kibiashara.
Nchi wajumbe kumi na mmoja wa Baraza la Usalama wamepiga kura kuunga mkono mswada huo, huku China na Russia zimepiga kura dhidi yake, na Colombia na Pakistan zikijizuia kupiga kura.
Kwenye ufafanuzi wake ya kura, Balozi Fu amesema mgogoro huo nchini Iran na athari zake zinazoenea zinaendelea kutoa pigo kubwa kwa amani na utulivu wa kikanda na kimataifa, zikiathiri uchumi wa dunia na kusababisha mivurugiko inayozidi kuenea.
"Marekani na Israel, bila idhini ya Baraza la Usalama na wakati mazungumzo kati ya Iran na Marekani yalikuwa yakiendelea, zilianzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran," amesema. "Hili ni ukiukaji wa wazi wa madhumuni na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa na kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa." ameongeza.
"Wakati huo huo, mamlaka, usalama, na ukamilifu wa ardhi wa Nchi za Ghuba lazima viheshimiwe kikamilifu. Raia na maeneo yasiyo ya kijeshi lazima yapewe ulinzi unaohitajika. Usalama wa njia za usafirishaji wa baharini na miundombinu ya nishati lazima pia ulindwe," Fu amesema.
Chini ya hali ya sasa, Fu Cong amesema,mswada huo unapaswa kubainisha wazi chanzo cha mgogoro huo, kutafuta suluhu mwafaka za kukabiliana nacho, na kuhakikisha usalama wa njia za usafirishaji wa baharini, na kuhimiza mazungumzo kwa ajili ya kufikia amani.
"Hata hivyo, inasikitisha kwamba mswada huo unashindwa kuakisi chanzo cha mgogoro na hali yake kamili kwa njia ya kina na yenye uwiano. Inajumuisha lawama na shinikizo la upande mmoja, pamoja na kuainisha hali hiyo kama tishio kwa amani na usalama wa kimataifa, vilevile matumizi ya usindikizaji wa silaha," amesema, akiongeza kuwa maneno hayo "yanaweza kutafsiriwa vibaya au hata kutumiwa vibaya."
Balozi Fu pia amesisitiza kwamba hatua za Baraza la Usalama zinapaswa kulenga kupunguza mvutano na "hazipaswi kutoa uhalali wa kisheria kwa operesheni za kijeshi ambazo hazijaidhinishwa."
“Baraza la Usalama halipaswi kuharakisha kupiga kura kuhusu mswada huo wakati wasiwasi mkubwa umeibuliwa na baadhi ya nchi wajumbe,” amesema. "Kwa kuzingatia hayo, China haikuwa na chaguo lingine ila kupiga kura dhidi ya mswada huo." Ameongeza.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma