Lugha Nyingine
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lashindwa Kupitisha mswada wa Azimio kuhusu Mlango Bahari wa Hormuz

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Fu Cong (katikati, mbele) akipika kura ya veto dhidi ya mswada wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Mlango Bahari wa Hormuz katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Aprili 7, 2026. (Xinhua/Xie E)
UMOJA WA MATAIFA - Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kupitisha mswada wa azimio ambalo "linahimiza sana" nchi zenye nia ya kutumia njia za kibiashara za usafirishaji wa baharini katika Mlango Bahari wa Hormuz kuratibu juhudi zenye muundo wa kujilinda ili kusaidia kuhakikisha usalama wa urambazaji katika Mlango Bahari wa Hormuz, ikiwemo kwa kusindikiza meli za kibiashara.
Nchi wajumbe kumi na mmoja wa Baraza la Usalama wamepiga kura kuunga mkono mswada wa azimio hilo, huku China na Russia zimepiga kura dhidi yake, na Colombia na Pakistan zikijizuia kupiga kura.
Mswada huo ulipendekezwa na Bahrain kwa uratibu na nchi wajumbe wenzake wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba GCC za Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia na Falme za Kiarabu, pamoja na Jordan.
Katika ufafanuzi wake wa kura, mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Fu Cong amesema mswada huo umeshindwa kuakisi chanzo cha mgogoro na hali yake kamili kwa njia ya kina na yenye uwiano.
"Baraza la Usalama halipaswi kuharakisha kupiga kura kuhusu mswada wa azimio wakati wasiwasi mkubwa umeibuliwa na baadhi ya wajumbe," Fu amesema.
Ameeleza matumaini kwamba amani na utulivu vitarejeshwa na kusisitiza kujitolea kwa China katika kushughulikia hali hiyo ipasavyo kwa kuzingatia chanzo chake.
"Vita hivi havikupaswa kutokea kamwe," Fu amesema, akizitaka Marekani na Israeli kusimamisha "hatua zao haramu za kijeshi."
Vassily Nebenzia, mjumbe wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa, amesema mswada huo umewasilisha hatua za Iran kama chanzo pekee cha mvutano ya kikanda, huku mashambulizi haramu ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran "hayakutajwa hata kidogo.”

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma