Lugha Nyingine
Kujenga Vipaji na Kutumia Kikamilifu Teknolojia katika Tiba za Jadi za China ili Kunufaisha Watu wa Afrika
Katika miaka ya hivi karibuni, China na nchi za Afrika zimeendeleza kwa kina ushirikiano wao katika sekta ya huduma za afya, zikipata matokeo mazuri kwenye mabadilishano ya Tiba za Jadi za China (TCM). Karakana ya Luban nchini Mali inatoa mafunzo ya TCM kwa wataalamu wenyeji, timu za madaktari wa China nchini Tanzania zinatoa huduma ya kupima na kutibu magonjwa kwa tiba hizo, na Afrika Kusini inatumia teknolojia ya AI kuongeza ufanisi wa tiba hizo za jadi za China. Hakika Tiba za Jadi za China zinaleta afya njema kwa watu wengi zaidi barani Afrika.
Karakana ya Luban ya Ujuzi wa Tiba za Jadi za China
"Kujitahidi Kujenga Vipaji Vingi Zaidi vya Wenyeji"
Katika Chuo cha Tiba cha Tianjin, Aaron Michael, mwanafunzi kutoka Mali mwenye umri wa miaka 25, alikuwa ameketi pamoja na wenzake wanne wakijadili waliyoyasoma darasani. “Je, kama mgonjwa akiwa na tatizo la maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo, sindano zinaweza kutumika katika pointi hizi za acupuncture kwa wakati mmoja?” Mmoja wao aliuliza swali, wakati wakitafuta majibu ya swali hilo, na kundi hilo la wanafunzi walisoma kitabu ili kupata majibu huku wakitumia ishara kuonesha sehemu za pointi hizo mwilini. Wanafunzi wote hao watano wanasoma katika Karakana ya Luban ya Ujuzi wa Tiba za Jadi za China ya Mali, na waliwasili Tianjin, China Desemba mwaka jana ili kuanza kozi ya mafunzo ya miaka mitatu inayojumuisha misingi ya kinadharia na matumizi ya kivitendo ya tiba hizo za jadi za China.
Mnamo mwezi Desemba, 2019, Chuo hicho cha Tiba cha Tianjin, Shule ya Sekondari ya Ufundi Stadi ya Hongxing ya Tianjin, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Bamako na Chuo Kikuu cha Sanaa na Sayansi cha Bamako zilianzisha kwa pamoja Karakana ya kwanza ya Luban mahsusi kwa ajili ya Tiba za Jadi za China duniani. "Tunadhamiria kutoa mafunzo ya ufundi stadi katika TCM (tiba za jadi za China) kwa vijana wa Mali, kuwezesha watu wengi zaidi kujua na kujifunza tiba za jadi za China" Diarra Boubacar, mwanzilishi wa karakana hiyo amewaambia waandishi wa habari.
Kwa sasa, karakana hiyo imeunda mfumo kamili wa kujenga vipaji. Katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Bamako, wanafunzi wanaweza kusoma tiba za jadi za China kama moja ya kozi ya hiari au kozi kuu. Katika kipindi cha miaka zaidi ya sita iliyopita, karakana hiyo kwa ujumla imetoa mafunzo ya vipaji husika kwa watu zaidi ya 1,000, miongoni mwao wanafunzi 54 kutoka Mali wamekuwa wataalamu wa tiba za jadi za China baada ya kukamilisha mafunzo ya kimfumo.
Timu ya Madaktari wa China nchini Tanzania
"Mbinu za Kupima na Kutibu Magonjwa kwa Tiba za Jadi za China Zaleta Matokeo ya Kasi na Yenye Ufanisi"
Katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Tanzania, mgonjwa aliyekuwa akisumbuliwa na maumivu ya muda mrefu ya shingo alikuwa amelala kwenye kitanda cha matibabu, wakati Chen Wenming, daktari wa timu ya 27 ya madaktari wa China nchini Tanzania alikuwa akinyoosha kwa upole sindano na kumfanyia tiba ya acupuncture, huku madaktari wa Tanzania wakiwa karibu na kurekodi kwa makini mambo muhimu ya vitendo. Katika mafunzo hayo, madaktari zaidi ya 30 kutoka idara tofauti walijifunza nadharia za kimsingi za tiba za jadi za China, njia za kawaida za kutibu magonjwa ya kawaida, na ufundi stadi kama vile acupuncture, masaji na tiba ya kutumia vikombe.
"Njia za kupima na kutibu magonjwa kwa Tiba za Jadi za China – kama vile acupuncture na masaji zinatoa matokeo kwa kasi na zina ufanisi sana, jambo ambalo ni la kuvutia sana." Amesema Mboma, mkuu wa idara ya upasuaji ya hospitali hiyo, akiongeza kuwa, mafunzo hayo yamepanua njia za matibabu, na yamehimiza zaidi ushirikiano wa kimatibabu kati ya Tanzania na China.
Tangu kuwasili Mbeya Oktoba, 2024, madaktari wa timu hiyo ya 27 ya madaktari wa China nchini Tanzania, wameingiza Tiba za Jadi za China kwenye huduma zao za matibabu za kila siku. Chen amewaelezea waandishi wa habari kuwa, kwa kutumia mbinu zao kulingana na halisi halisi ya kila mgonjwa, madaktari wa timu hiyo hutumia matibabu ya Tiba za Jadi za China - kama vile Moxibustion - kusaidia wagonjwa wengi wenye matatizo ya orthopediki na maumivu sugu kupoza maumivu yao na kuboresha afya zao.
Kituo cha Tiba za Jadi za China na Acupuncture cha Afrika nchini Afrika Kusini
“Teknolojia ya AI Inaleta Uwezekano Mkubwa Zaidi kwa Tiba za Jadi za China”
Katika Kituo cha Tiba za Jadi za China na Acupuncture cha Afrika huko Johannesburg, Afrika Kusini, Christine, mwenye umri wa miaka 26 kutoka Afrika Kusini, alikuwa akiongozwa na wahudumu kuelekea kwenye kifaa cha kupima afya kwa Tiba ya Jadi ya China kinachowezeshwa na AI, ambapo alifuata maelekezo ya kwenye skrini kupigwa picha ya uso na ulimi wake. Dakika chache baadaye, ripoti ya matokeo ya vipimo hivyo - inayojumuisha uchambuzi kamili na mapendekezo ya afya yake - ilitokea kwenye skrini ya kifaa hicho.
"Una tatizo la upungufu wa Qi na damu, likiambatana na vizuizi kwenye njia za mabega na shingo yako." Hu Zijing, mkurugenzi wa kituo hicho ambaye pia ni profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Johannesburg, alimwelezea hilo Christine hatua kwa hatua, kuanzia mwonekano wa ulimi wake hadi hali ya njia zake.
Kituo hicho ni msingi wa kivitendo kwa tiba ya acupuncture katika Chuo Kikuu cha Johannesburg. Katika miaka ya hivi karibuni, kituo hicho kimeingiza vifaa vya kupima na kutibu vinavyowezeshwa na AI kwa ajili ya Tiba za Jadi za China, ambayo imeongeza ufanisi kwenye mchakato wa kupima na kutibu.
(Majina yote ya watu yaliyotajwa katika makala hii yametafsiriwa katika Kiswahili kutoka maandishi ya asili ya Kichina kwa kuzingatia namna yanavyotamkwa.)

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma