Rais wa Rwanda ahimiza kuwa macho dhidi ya ukataaji wa mauaji ya kimbari

(CRI Online) April 08, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais wa Rwanda Paul Kagame jana Jumanne alisisitiza umuhimu wa kukabiliana na ukataaji wa mauaji ya kimbari na kuhifadhi ukweli wa kihistoria wakati ambapo nchi hiyo imeanza wiki ya maombolezo ya kitaifa na siku 100 za maadhimisho ya kumbukizi ya 32 ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya watutsi.

Rais Kagame na mke wake Jeannette Kagame, pamoja na mkuu wa kundi la wanadiplomasia nchini Rwanda, waliweka mashada ya maua katika Jumba la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari mjini Kigali, ambako waathirika zaidi ya laki 2.5 walizikwa.

Rais Kagame amesema uhalisia wa mauaji ya kimbari uko wazi kwa wote kuona, na kwamba viongozi halisi walihukumiwa katika mahakama za kitaifa kwa ushahidi thabiti, na mchakato wa Gacaca ulirekodi sababu za mauaji hayo kwa namna ambayo haikuwahi kuonekana au kusikika nchini Rwanda.

“Ukweli hauwezi kukataliwa, lakini baadhi ya watu wanaendelea kupotosha uhalisia” Rais Kagame amesema, akionya kuwa kupuuza huko kunaweza kuongeza hatari ya kujirudia kwa historia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha