Uganda yatangaza msamaha wa viza kwa wageni wakati wa kipindi cha AFCON 2027

(CRI Online) April 08, 2026

Serikali ya Uganda imetangaza msamaha wa visa kwa wageni watakaosafiri kwenda nchini humo wakati wa kipindi cha Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.

Uganda itaandaa mashindano hayo kwa pamoja na Kenya na Tanzania kuanzia tarehe 19 Juni hadi tarehe 18 Julai mwaka 2027.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya AFCON nchini Uganda Dennis K. Mugimba ametoa tangaza hilo jana Jumanne kwenye mkutano na wanahabari mjini Kampala.

“Baraza la Mawaziri la serikali ya Uganda limeamua kutoa msamaha wa viza kwa wageni wanaokuja Uganda, kuanzia mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa AFCON 2027 na kuisha mwezi mmoja baada ya michezo hiyo. Uamuzi huu unalenga kuhamasisha wageni wengi zaidi kuja Uganda kama sehemu ya kutangaza na kunadi Kutembelea Uganda.” Mugimba amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha