Lugha Nyingine
Rais Xi asisitiza kuzidisha marekebisho ya kisiasa kwa kina, kwenye semina ya mafunzo kwa maofisa wa jeshi

Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihutubia semina ya mafunzo kwa maofisa wa ngazi za juu wa jeshi, Beijing, mji mkuu wa China, Aprili 8, 2026. (Xinhua/Li Gang)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amehimiza juhudi za kuzidisha marekebisho ya kisiasa kwa kina katika jeshi ili kudumisha usafi na ufahari wa jeshi la umma.
Rais Xi, ameyasema hayo jana Jumatano wakati akihutubia hafla ya kuanzishwa kwa semina ya mafunzo kwa maofisa wa ngazi za juu wa jeshi, iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Ulinzi wa Taifa mjinii Beijing siku hiyo.
Ametoa wito wa kuwataka kuwa na mtazamo mpya wa kisiasa ili kukaribisha maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, ambayo yataadhimishwa mwaka 2027.
Rais Xi akisisitiza umuhimu wa kuwa na matumaini na imani, amesema kuwa mmoja wa Chama na jeshi kunamaanisha kuwa na imani thabiti juu ya Umarksi na kutii Chama . Ametoa wito wa kuwataka maofisa hao wa ngazi za juu wa jeshi wawe watangulizi katika kuanzisha kwa makini shughuli za kisiasa ndani ya chama, na kutafuta ukweli wa mambo kwa kufuata hali halisi.
"Mawazo au vitendo vyote vinavyotokana na maslahi binafsi na ufisadi haviendani kabisa na hali na nia ya Chama," Rais Xi amesema.
Rais Xi pia amehimiza maofisa hao wa ngazi za juu wa jeshi wawe watangulizi katika kurejesha na kufuata desturi za ufahari za Chama na jeshi, kuacha mienendo ya umangimeza, na kudumisha hali asili ya wanajeshi wahudumu wa kimapinduzi.
Rais Xi amesema kila mmoja ni sawa mbele ya sheria na kanuni, na hakuna hali maalum katika kufuata sheria na kanuni, na hakuna upekee katika utekelezaji wa sheria.
Rais Xi ameeleza imani kwamba katika hali mpya ya kihistoria, jeshi litakuwa na mshikamano na umoja usio na kifani na litaandika ukurasa mpya wa kujenga jeshi lenye nguvu kubwa.
Zhang Shengmin, naibu mwenyekiti wa CMC, aliongoza hafla hiyo ya kuanzishwa kwa semina ya mafunzo.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma