Mwenyekiti wa KMT atoa heshima katika Kaburi la Sun Yat-sen mjini Nanjing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2026

Cheng Li-wun, mwenyekiti wa chama cha Kuomintang (KMT), akiongoza ujumbe wa KMT kutoa heshima katika Kaburi la Sun Yat-sen, Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Aprili 8, 2026. (Xinhua/Xing Guangli)

NANJING - Cheng Li-wun, mwenyekiti wa chama cha Kuomintang (KMT), ameongoza ujumbe wa KMT Jumatano asubuhi kutoa heshima katika Kaburi la Sun Yat-sen mjini Nanjing, mji mkuu wa Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China.

Sun alikuwa mmoja wa mwanzilishi wa chama cha KMT. Kutoa heshima katika kaburi lake kumekuwa sehemu muhimu ya ziara za wenyeviti wa chama hicho wanapotembelea China Bara.

Cheng na wajumbe wengine wa ujumbe huo, wakiwemo makamu wenyeviti watatu wa KMT -- Lee Chien-lung, Chang Jung-kung na Hsiao Hsu-tsen, walisimama kwa heshima mbele ya sanamu ya Sun Yat-sen iliyochongwa kwa marumaru nyeupe akiwa ameketi. Cheng aliweka shada la maua ya manjano. Wajumbe wa ujumbe huo waliinama mara tatu na kutoa heshima kwa ukimya.

Ujumbe huo kisha ulitembelea chumba ambako jeneza la Sun limehifadhiwa.

Sun, kiongozi wa mapinduzi anayeheshimiwa ambaye alichukua nafasi muhimu katika kupindua utawala wa kifalme nchini China, alifariki mwaka 1925. Mwili wake ulizikwa kwenye kaburi hilo mwaka 1929.

Cheng ni mwenyekiti wa kwanza wa KMT katika miaka 10 ambaye ameongoza ujumbe kwenda China Bara. Ziara yake hiyo inaonekana kuwa sehemu muhimu ya mawasiliano na mazungumzo kati ya KMT na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika mazingira mapya.

Cheng amesema ziara yake hiyo inalenga "kupanda mbegu ya amani" miongoni mwa Wachina wa pande zote mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan. Ametoa wito wa juhudi za pamoja za "kumwagilia na kurutubisha mbegu hiyo ili ikue na kuwa mti mrefu."

Suala la Taiwan ni athari iliyosalia kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopiganwa kati ya vikosi vilivyoongozwa na CPC na KMT takriban miongo minane iliyopita. Mwaka 1949, sehemu iliyokuwa imebaki ya KMT iliyoshindwa kwenye vita hivyo ilijiondoa kwenda Taiwan, na Jamhuri ya Watu wa China (PRC) ilianzishwa rasmi chini ya uongozi wa CPC.

Vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo havijapatiwa ufumbuzi pamoja na uingiliaji wa nje vimeziacha pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan katika hali ya mvutano wa kisiasa wa muda mrefu. Hata hivyo, ukweli kwamba Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya China haujawahi kubadilika.

Mwaka 1971, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio No. 2758 kwa wingi mkubwa, likifafanua kwamba serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ndiyo serikali pekee halali inayowakilisha China. Inatambuliwa kwa upana na jumuiya ya kimataifa kwamba kuna China moja tu na kwamba Taiwan ni sehemu ya China.

Cheng aliwasili Shanghai Jumanne. Ziara yake hiyo, ambayo inajumuisha Jiangsu, Shanghai na Beijing, itaendelea hadi Jumapili. 

Cheng Li-wun, mwenyekiti wa chama cha Kuomintang (KMT), akiongoza ujumbe wa KMT kutoa heshima katika Kaburi la Sun Yat-sen, Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Aprili 8, 2026. (Xinhua/Xing Guangli)

Cheng Li-wun, mwenyekiti wa chama cha Kuomintang (KMT), akiongoza ujumbe wa KMT kutoa heshima katika Kaburi la Sun Yat-sen, Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Aprili 8, 2026. (Xinhua/Xing Guangli)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha