Afrika Kusini yakaribisha makubaliano ya kusimamisha mapigano juu ya mgogoro wa Iran

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2026

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akizungumza wakati akihutubia wanadiplomasia waliowasilisha barua za utambulisho wa  wakuu wapya wa misheni walioteuliwa nchini Afrika Kusini kwenye jumba la wageni wa rais, Pretoria, Afrika Kusini, Aprili 8, 2026. (GCIS/kupitia Xinhua)

JOHANNESBURG - Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekaribisha makubaliano ya kusimamisha mapigano kuhusu mgogoro wa Iran, akisema ni hatua muhimu kuelekea utulivu wa kikanda.

Ramaphosa ametoa kauli hiyo Jumatano asubuhi kwenye jumba la wageni wa rais mjini Pretoria, alipokuwa akihutubia wanadiplomasia waliowasilisha barua za utambulisho wa wakuu wapya wa misheni walioteuliwa nchini Afrika Kusini.

Mgogoro huo ulizuka Februari 28, wakati Marekani na Israeli zilipoanzisha mashambulizi ya anga ya pamoja yaliyolenga miundombinu na uongozi wa Iran. Iran ilijibu kwa mashambulizi ya kulipiza kwa kutumia makombora na droni, pamoja na kuufunga Mlango Bahari wa Hormuz.

Kufuatia juhudi za upatanishi za nchi kama vile Pakistan, makubaliano ya kusimamisha mapigano kwa wiki mbili yalitangazwa Jumanne jioni.

"Tunatambua mipango ya sasa na juhudi zinazoendelea yenye lengo la kufikia mwisho kamili wa mgogoro huo katika eneo la Mashariki ya Kati. Tunakaribisha tangazo la kusimamisha mapigano na tunatumaini kwamba litaweka msingi wa suluhu ya kudumu," Ramaphosa amesema.

"Afrika Kusini kwa mara nyingine tena inatoa wito wa mazungumzo na upatanishi ili kuzuia upotevu zaidi wa maisha na uharibifu wa mali, na kuhakikisha amani ya haki, endelevu na ya kudumu. Aidha, tunatoa wito kwa nchi zote kuheshimu sheria za kimataifa na mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa nchi zote," rais huyo amesema

Amebainisha kuwa Afrika Kusini inatetea utaratibu wa kimataifa unaojengwa juu ya amani na urafiki miongoni mwa nchi zote duniani, akizihimiza nchi kuungana dhidi ya "ubaguzi wa rangi, ukoloni, utumwa na aina zote za ukandamizaji na kutovumiliana."

"Tunajitahidi kuhakikisha kwamba amani na usalama duniani vinadumishwa kupitia mazungumzo na majadiliano, si kwa kutumia nguvu za silaha," rais huyo amesema, akitoa wito kwa pande zote kuheshimu sheria za kimataifa na mamlaka ya kitaifa.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akizungumza wakati akihutubia wanadiplomasia waliowasilisha barua za utambulisho wa wakuu wapya wa misheni walioteuliwa nchini Afrika Kusini kwenye jumba la wageni wa rais, Pretoria, Afrika Kusini, Aprili 8, 2026. (GCIS/kupitia Xinhua)

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akizungumza wakati akihutubia wanadiplomasia waliowasilisha barua za utambulisho wa wakuu wapya wa misheni walioteuliwa nchini Afrika Kusini kwenye jumba la wageni wa rais, Pretoria, Afrika Kusini, Aprili 8, 2026. (GCIS/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha