Lugha Nyingine
COMESA yapitisha mkakati wa kuhimiza utekelezaji wa AfCFTA
Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) limeridhia mkakati wa kusaidia nchi wanachama wake kutekeleza kwa ufanisi Eneo la Biashara Huria Barani Afrika (AfCFTA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano, mkakati huo umepitishwa kwenye mkutano maalumu wa tisa wa baraza la mawaziri uliofanyika Aprili 2, ambao pia umepitisha Mpango Mkakati wa Kipindi cha Kati wa COMESA kwa 2026-2030.
Taarifa hiyo imesema mkakati huo unatoa mbinu ya kimfumo inayowezesha nchi wanachama kutumia fursa za soko la bara hilo, huku zikiimarisha jukumu la COMESA la kuwa mjenzi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika.
Mkutano huo umesisitiza tena dhamira ya COMESA katika kuhimiza mafungamano ya kikanda, na kuendeleza jukumu lake ndani ya mfumo mpana wa maendeleo ya bara.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma