Lugha Nyingine
AU yaadhimisha mauaji ya kimbari ya Rwanda kwa uzinduzi wa kumbukumbu ya mtandaoni
Umoja wa Afrika (AU) umeadhimisha kumbukizi ya miaka 32 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda, kwa kuzindua kumbukumbu ya mtandaoni, kuenzi waathirika zaidi ya milioni moja.
Hafla maalum iliyopewa jina la "Kwibuka-32", ikimaanisha "kukumbuka", ilifanyika Jumanne katika makao makuu ya AU yaliyopo Addis Ababa nchini Ethiopia, na kuwaleta pamoja viongozi wa AU, wajumbe wa kidiplomasia, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa, viongozi wa kidini, pamoja na wajumbe wa jamii ya Rwanda nchini Ethiopia.
Akihutubia tukio hilo la kumbukizi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Mahmoud Ali Youssouf alisema chuki iliyopangwa haitaruhusiwa tena kuwa mradi wa kisiasa, akisisitiza kwamba sasa wanakumbuka zaidi ya watu milioni moja waliopoteza maisha kwa chuki, kutojali, na kutochukua hatua. Aidha amesema Kwibuka si wakati wa maombolezo tu, bali pia ni wito wa ukweli, uwajibikaji, na tahadhari.
Pia umoja huo ukishirikiana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa katika AU, umezindua Kumbukumbu ya Haki za Binadamu ya Mtandaoni ya AU, ambayo ni chumba cha mtandaoni kinachohusu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma