Rais wa China atoa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya China na Uhispania kwa ajili ya mafanikio mengi zaidi

(CRI Online) April 15, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza haja kwa China na Uhispania kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara, nishati mpya na uchumi janja, na kuhimiza mawasiliano katika utamaduni, elimu, utafiti wa kisayansi na michezo.

Rais Xi ameyasema hayo wakati alipokutana na waziri mkuu wa Uhispania Bw. Pedro Sanchez ambaye yuko ziarani nchini China.

Akisema kuwa China na Uhispania zinatakiwa kuchangamkia fursa na kutafuta maendeleo yanayoendeshwa kwa kutegemea uvumbuzi, Rais Xi amemwambia Bw. Sanchez kuwa nchi mbili zinatakiwa kukuza uhusiano wa kimkakati wa pande zote ili kuzalisha matokeo mengi zaidi na kuleta manufaa zaidi kwa watu wao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha