Rais wa China atoa pendekezo lenye vipengele vinne kuhusu kuhimiza amani na utulivu katika Mashariki ya Kati

(CRI Online) April 15, 2026

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa pendekezo lenye vipengele vinne kuhusu kuhimiza amani na utulivu katika Mashariki ya Kati, wakati alipokutana na Sheikh Khaled bin Mohamed bin Zayed Al Nahyan, mwana mfalme wa Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu hapa Beijing.

Rais Xi ametoa mwito wa kushikilia kanuni za kuishi pamoja kwa amani. Amesisitiza umuhimu wa kuhimiza ujenzi wa mfumo wa usalama ulio endelevu, wa pamoja, wa pande zote na wenye ushirikiano kwa Mashariki ya Kati na Nchi za Ghuba.

Akizungumzia kanuni ya usimamizi wa sheria wa kimataifa, rais Xi amesema kanuni ya usimamizi wa sheria wa kimataifa inatakiwa kuimarishwa ili kuzuia dunia isitumbukie tena katika sheria ya msituni ambayo wenye nguvu ndio wanawatawala wanyonge. Amesema, maendeleo na usalama vinatakiwa kuratibiwa. Pande zote zinatakiwa kufanya juhudi kwa pamoja ili kujenga mazingira wezeshi kwa maendeleo ya nchi za Mashariki ya Kati na Eneo la Ghuba.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha