Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Pakistan
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi tarehe 13 Aprili amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Bw. Muhammad Ishaq Dar.
Bw. Dar ameeleza kwa kina kuhusu juhudi za usuluhishi za Pakistan kwenye mazungumzo kati ya Iran na Marekani, akiishukuru China kwa juhudi zake katika kuhimiza amani, na kueleza kuwa Pakistan inapenda kufanya mawasiliano na ushirikiano wa karibu na China, na kutoa mchango kwa pamoja kwa ajili ya kutimiza amani ya kikanda. Bw. Wang amesisitiza tena msimamo wa kikanuni wa China, akiipongeza Pakistan kwa kusaidia kutimiza usitishwaji vita wa muda kati ya Marekani na Iran na kuandaa mazungumzo ya Islamabad, na kusema Pakistan imefanya kazi ya usuluhishi yenye haki na usawa. Wang amesema jambo muhimu kwa sasa ni kuepuka kuanza tena kwa mapigano. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuendelea na juhudi za kuhimiza maafikiano na mazungumzo, na kupinga wazi kitendo chochote kinachoharibu usitishwaji vita na kuchochea mapigano kupamba moto.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma