Lugha Nyingine
Sekta ya parachichi nchini Kenya kufaidika na sera ya ushuru sifuri ya China
Mnyororo wa thamani wa parachichi nchini Kenya, unaoanzia kwa wakulima, wavunaji, wachakataji na wauzaji, una matarajio mazuri kwamba, sera ya ushuru sifuri itakayoanza kutekelezwa Mei Mosi, 2026, itafungua fursa muhimu kwa sekta hiyo.
Kenya, nchi inayoongoza kwa mauzo ya nje ya parachichi aina ya Hass, ni kati ya nchi 53 za Afrika zinazotarajiwa kufaidika na sera hiyo itakayowawezesha kuingia kwenye soko la China, hatua inayoboresha ushindani na thamani ya mauzo yake.
Ofisa mwandamizi mkuu wa Jamii ya Wakulima wa Parachichi nchini Kenya Ernest Muthomi amepongeza hatua ya kuondoa ushuru, akisema itachochea mauzo ya zao hilo nchini China na kuleta faida kwa wakulima na wavunaji wa Kenya.
Ameongeza kuwa, kampuni kadhaa za China tayari zimeanzisha viwanda vya uchakataji nchini Kenya kuzalisha mafuta ya parachichi kwa ajili ya kuuza nchini China, na kutoa nafasi za ajira na kuongeza thamani katika sekta hiyo.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma