Lugha Nyingine
Mradi wa kilimo wa FAO, China na Uganda wathibitisha mafanikio ya ushirikiano wa Kusini na Kusini
Maofisa wanaoshiriki katika semina ya kukamilika kwa awamu ya tatu ya Ushirikiano kati ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), China na Uganda wamesema, uhamishaji wa ujuzi na teknolojia wa China unaleta mabadiliko katika uzalishaji wa kilimo nchini Uganda, ukionyesha jinsi nchi za Dunia ya Kusini zinavyoweza kuongeza kasi ya maendeleo kupitia ushirikiano wa Kusini na Kusini.
Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ya Uganda, tangu mradi huo ulipoanza mwaka 2012, China imepeleka zaidi ya wataalamu 60 wa kilimo nchini Uganda kubadilishana uzoefu na ujuzi na wakulima wadogo na wataalam wa huko, kuwasaidia wakulima wa Uganda kubadilika kutoka kilimo cha kujikimu hadi kilimo cha kibiashara, na kuongeza uzalishaji na kipato kwa familia.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Uganda Frank Tumwebaze amesema, mradi huo umeonyesha jinsi nchi za Dunia ya Kusini zinavyoweza kufanya uratibu wa kubadilishana uzoefu na teknojia ili kubadili mifumo yao ya chakula na kilimo.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma