Lugha Nyingine
Rais Xi asema usafirishaji wa kawaida kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz unapaswa kudumishwa
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatatu katika mazungumzo kwa njia ya simu na Mwanamfalme ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Al Saud amesema kwamba usafirishaji wa kawaida kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz unapaswa kudumishwa.
Rais Xi amesema kwamba China inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano na Saudi Arabia na siku zote inafuata kanuni za kuheshimiana, kuwa na usawa na kunufaishana.
Akisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Saudi Arabia, Rais Xi amesema China ina nia ya kushirikiana na Saudi Arabia ili kutumia ipasavyo fursa hiyo kuzidisha hali ya kuaminiana kimkakati, kuimarisha ushirikiano wa kufuata hali halisi, na kuboresha mawasiliano katika ngazi zote, ili kupanua hatua kwa hatua upana na kina cha uhusiano wa pande mbili na kuweka mfano kwa ajili ya kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China na nchi za Kiarabu.
Kuhusu hali ya hivi sasa katika Mashariki ya Kati na eneo la Ghuba, Rais Xi amesisitiza kwamba China inatoa wito wa kusimamisha mara moja mapigano kwa pande zote na kukomesha uhasama, inaunga mkono juhudi zote zinazosaidia kurejesha amani, na inajitahidi zaidi katika kutatua migogoro kwa kupitia njia za kisiasa na kidiplomasia.
Rais Xi amesema kwamba usafirishaji wa kawaida kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz unalingana na maslahi ya pamoja ya nchi za kikanda na jumuiya ya kimataifa, na ameongeza kuwa China inaunga mkono nchi za kikanda katika kujenga maskani ya pamoja yaliyo ya ujirani mwema, maendeleo, usalama na ushirikiano, kujenga siku zao za baadaye na mustakabali wao wenyewe, na kuhimiza amani na utulivu wa muda mrefu katika eneo hilo.
Kwa upande wake, Mohammed amesema kwamba uhusiano kati ya Saudi Arabia na China ni wa kimkakati, na kuendeleza uhusiano na China ni muhimu sana kwa nchi yake, na amedhihirisha kuwa mgogoro wa sasa katika Mashariki ya Kati umeharibu usalama wa nchi za Ghuba na unaathiri vibaya utoaji wa nishati na uendeshaji wa uchumi duniani.
"Saudi Arabia inapenda kuongeza mawasiliano na uratibu na China, kudumisha usimamishaji mapigano ulio wa sasa, kuzuia kurudia tena kwa mgogoro, kuhakikisha usafirishaji salama na huria kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, na kutafuta kwa pamoja njia za kufikia amani na utulivu wa muda mrefu katika eneo hilo," amesema Mohammed.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma