Lugha Nyingine
Trump asema "hakuna uwezekano mkubwa" wa kuongeza muda wa kusimamisha mapigano na Iran
WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amesema "hakuna uwezekano mkubwa" kwamba ataongeza muda wa kusimamisha mapigano kwa wiki mbili na Iran kama makubaliano hayatafikiwa kabla ya kumalizika wiki hii, kwa mujibu wa ripoti ya chombo cha habari cha Bloomberg jana Jumatatu.
"Mlango-Bahari wa Hormuz utaendelea kuzuiwa hadi makubaliano ya amani yatakapokamilishwa,” Trump amesema katika mahojiano kwa njia ya simu.
"Wanataka niufungue. Wairani wanataka sana ufunguliwe. Sitaufungua hadi makubaliano yatakaposainiwa," amesema.
Bei za mafuta zimepanda wakati ambapo Washington inaendelea kuuzuia mlango-bahari huo na Kikosi cha Majini cha Jeshi la Marekani kikikamata meli yenye kupeperusha bendera ya Iran mwishoni mwa wiki iliyopita.
"Sitaharakishwa kuingia katika kufanya makubaliano mabaya. Tuna muda wote duniani," Trump amesema.
Amesema makubaliano ya kusimamisha mapigano, ambayo aliyatangaza Aprili 7, yataisha muda wake kesho Jumatano jioni kwa Saa za Mashariki za Marekani.
Alipoulizwa kama anatarajia mashambulizi kuanza tena mara moja baada ya hapo kama hakuna makubaliano yatakuwa yamefikiwa, Trump amesema: "Kama hakuna makubaliano yatakuwa yamefikiwa, hakika ninatarajia."
Katika mahojiano kwa njia ya simu na Shirika la Habari la Marekani (PBS) jana Jumatatu asubuhi, Trump amesema kwamba kama makubaliano ya kusimamisha mapigano na Iran yataisha muda wake, "basi mabomu mengi yataanza kufyatuliwa."
Alipoulizwa kama wapatanishi wa Iran watashiriki kwenye mazungumzo mapya mjini Islamabad, Trump amesema: "Sijui. Ninamaanisha, wanatakiwa kuwepo. Tulikubaliana kuwepo huko, ingawa wanasema hatukukubaliana. Lakini hapana, yalikuwa yameshapangwa. Na tutaona kama yatakuwepo au la. Kama hayatakuwepo, hiyo ni sawa pia."
Ameliambia Gazeti la New York Post jana Jumatatu asubuhi kwamba Makamu Rais wa Marekani JD Vance anatarajiwa kuelekea Pakistan kwa ajili ya duru hiyo ya pili ya mazungumzo na maafisa wa Iran.
Hadi kufikia Jumatatu asubuhi, vikosi vya Marekani vilikuwa vimesharudisha meli 27 kuingia au kutoka bandari za Iran, Kamandi ya Mashariki ya Kati ya Marekani imesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma