Lugha Nyingine
Marais wa China na Msumbiji wafanya mazungumzo na kukubaliana kupandisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili

Rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha pamoja na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Daniel Francisco Chapo na mkewe Gueta Chapo kabla ya mazungumzo kati ya Xi na Chapo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 21, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Msumbiji Daniel Francisco Chapo wamefanya mazungumzo mjini Beijing jana Jumanne, na wakuu hao wawili wa nchi wamekubaliana kupandisha uhusiano wa nchi hizi mbili kuwa jumuiya ya China na Msumbiji yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.
Rais Xi akisema kuwa urafiki uliothaminiwa kwa muda mrefu kati ya China na Msumbiji umeweka mfano kwa uhusiano kati ya China na nchi za Afrika na ushirikiano wa Kusini na Kusini, amesema kwamba katika hali mpya ya sasa, kuzidisha ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Msumbiji kunalingana na matarajio ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili na kunaakisi mwelekeo uliopo kwa Nchi za Dunia ya Kusini kuimarisha mshikamano na ushirikiano katika kukabiliana na changamoto kwa pamoja.
"Urafiki na kuaminiana ni sifa wazi na nguvu bora ya kisiasa za uhusiano kati ya China na Msumbiji," Rais Xi amesema, akiongeza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kuendelea kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi ya kimsingi na masuala makubwa yanayofuatiliwa ya kila mmoja, kuhimiza mawasiliano kwenye ngazi mbalimbali na sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali, vyama vya siasa, vyombo vya kutunga sheria na mawasiliano kati ya serikali za mitaa, na kubadilishana na kunufaishana na uzoefu kuhusu ujenzi wa chama na utawala wa nchi.
Rais Xi amesisitiza kuwa,"kwa kukabiliwa na hali ya kimataifa yenye utatanisha na mabadiliko mengi, nchi zetu mbili zinapaswa kuendelea kuongeza uratibu na ushirikiano ndani ya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine, kuwa na mshikamano na ushirikiano, kutetea dunia yenye ncha nyingi iliyo ya usawa na utaratibu na utandawazi wa kiuchumi wenye manufaa na ulio jumuishi kwa wote, na kulinda kwa pamoja haki na usawa wa kimataifa.”
"Kutokana na athari za mgogoro wa Mashariki ya Kati kuenea katika nchi za Afrika, China inapenda kushirikiana na Afrika katika kukabiliana na changamoto hizi, kuhimiza amani kwa pamoja na kusukuma mbele maendeleo," Rais Xi amesema, akitoa wito kwa pande zote mbili kushikilia kanuni za amani, kudumisha azma kwa ajili ya maendeleo, na kuhimiza ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili.
Kwa upande wake, Rais Chapo amesema kuwa ni furaha kubwa kuwa kiongozi wa kwanza wa nchi ya Afrika kufanya ziara ya kiserikali nchini China mwaka huu. Ameipongeza China kwa mafanikio makubwa yanayosifiwa, na pia amepongeza kazi ya kielelezo inayofanywa na China kwa nchi za Dunia ya Kusini.
"Msumbiji inatilia maanani sana uhusiano wake na China, inafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja bila masharti, na inaiunga mkono China kufikia muungano wa taifa," Rais Chapo amesema.
Ameeleza kuwa Msumbiji inapenda kufanya ushirikiano na China kwenye msingi wa kuheshimiana na kuaminiana, ili kuimarisha mshikamano na urafiki.
Pande hizo mbili zimetoa Taarifa ya Pamoja ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Msumbiji juu ya Kujenga Jumuiya ya China na Msumbiji yenye Mustakabali wa Pamoja katika Zama Mpya.
Kabla ya mazungumzo hayo, Rais Xi na mkewe Peng Liyuan walifanya hafla ya kumkaribisha Rais Chapo na mkewe, Gueta Chapo, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Rais Xi na mkewe Peng pia walifanya tafrija ya kumkaribisha Rais Chapo na mkewe Gueta Chapo jana Jumanne jioni.

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Daniel Francisco Chapo, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 21, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Daniel Francisco Chapo kabla ya mazungumzo yao kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 21, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Daniel Francisco Chapo kabla ya mazungumzo yao kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 21, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma