Wataalamu wa China na Afrika watoa wito wa kuendeleza kwa kina ujenzi wa miundombinu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2026

Wageni  wakishiriki kwenye shughuli iliyofanyika katika wakati wa Mkutano wa kwanza wa Wajasiriamali wa China na Afrika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa, Ethiopia, Aprili 21, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

Wageni wakishiriki kwenye shughuli iliyofanyika wakati wa Mkutano wa kwanza wa Wajasiriamali wa China na Afrika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa, Ethiopia, Aprili 21, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

ADDIS ABABA - Maofisa na wataalamu kutoka China na Afrika wametoa wito wa kuzidisha zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika katika ujenzi wa miundombinu, na kusisitiza kuwa sekta binafsi inapaswa kufanya kazi ya uongozi katika kupunguza pengo linalozidi kuwa kubwa katika mendeleo ya miundombinu barani Afrika.

Wito huo umetolewa Jumanne wiki hii kwenye shughuli iliyofanyika wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wajasiriamali wa China na Afrika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.

Mkutano huo umekutanisha pamoja wajumbe wa kampuni maarufu za China zinazofanya shughuli zao barani Afrika, maofisa wa AU, na wataalamu wa China na Afrika kuhusu maendeleo ya miundombinu.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo, Wang Ligui, konsuli wa Ujumbe wa China ulioko katika AU, ametoa wito wa kuimarisha hali ya kuhusisha kimkakati Mpango wa Maendeleo ya Miundombinu barani Afrika unaoongozwa na AU na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China ili kuharakisha maendeleo ya miundombinu barani humo.

Nelisiwe Siphelele Mathabela, mkuu wa kitengo cha mambo ya utawala na usimamizi wa miundombinu katika Kamati ya AU, amesema kwamba ushirikiano kati ya Afrika na China katika miundombinu ni msingi wa uhusiano wa washirika wa Afrika na China, ukisukuma mbele maendeleo ya viwanda na ongezeko la uchumi barani Afrika.

Mathabela amesema kuwa China siku zote ni mshirika unaoongoza wa ujenzi wa miundombinu barani Afrika, na ni chanzo muhimu cha mitaji ya ujenzi wa miundombinu barani Afrika, na barabara kuu, reli na miradi ya nishati vikiwa vimefadhiliwa kupitia FOCAC au taasisi zake za mambo ya fedha.

Ban Yongzhi, mwakilishi mkuu wa Ofisi ya Kusini-Mashariki mwa Afrika ya Benki ya ExIm ya China, amesisitiza umuhimu mkubwa wa kufikiria mfumo na utaratibu, upangaji wa mpango wa jumla, na mfumo bora wa kukusanya mitaji ili kujenga mazingira ya maendeleo endelevu ya miundombinu.

Wageni  wakishiriki kwenye shughuli iliyofanyika katika wakati wa Mkutano wa kwanza wa Wajasiriamali wa China na Afrika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa, Ethiopia, Aprili 21, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

Wageni wakishiriki kwenye shughuli iliyofanyika wakati wa Mkutano wa kwanza wa Wajasiriamali wa China na Afrika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa, Ethiopia, Aprili 21, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha