Rais wa China ahimiza juhudi za kufanya vizuri majumuisho na kutumia ipasavyo “uzoefu wa maendeleo wa Yiwu” mashariki mwa China

(CRI Online) April 24, 2026

Rais Xi Jinping wa China amehimiza juhudi za kufanya vizuri majumuisho kuhusu uzoefu wa maendeleo wa mji wa Yiwu katika mkoa wa Zhejiang mashariki mwa China, na kuutumia vyema.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi (CMC), alisema hayo katika maagizo ya hivi karibuni.

Rais Xi amesema bidhaa ndogo za Yiwu zimeingia kwenye soko pana na kuwa sekta kubwa, na kuunda “uzoefu wa maendeleo wa Yiwu”, huu ni uzoefu uliofanywa kwa mafanikio katika kukuza uchumi wa maeneo ya wilaya kwa kufuata hali halisi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha