Kongamano kuhusu Maonesho ya 9 ya CIIE na Jukwaa la Hongqiao latoa mwito wa kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika

(CRI Online) April 24, 2026
Kongamano kuhusu Maonesho ya 9 ya CIIE na Jukwaa la Hongqiao latoa mwito wa kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika
(Picha/Xinhua)

Kongamano la ngazi ya juu kuhusu Maonesho ya 9 ya Uagizaji Bidhaa ya Kimataifa ya China (CIIE) na Jukwaa la tisa la Uchumi la Kimataifa la Hongqiao (HQF) lilifanyika Jumanne katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, likisisitiza haja ya kutumia vizuri majukwaa haya "maalum na yenye nguvu" ili kuingia kwenye soko kubwa la China na kuharakisha ukuaji wa viwanda barani Afrika.

Kongamano hilo la ngazi ya juu liliandaliwa kwa pamoja na Idara ya CIIE na Sekritarieti ya Jukwaa la Hongqiao, kwa ushirikiano na Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika na Kamisheni ya umoja huo. Kongamano hilo liliwakutanisha pamoja wageni 80, wakiwemo viongozi wa Umoja wa Afrika, maofisa wa China na Afrika, na wajumbe wa jumuiya ya biashara kutoka pande zote mbili, kwa lengo la kutafuta njia halisi za kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.

Akihutubia kongamano hilo, mkurugenzi wa viwanda, madini, ujasiriamali na utalii katika Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Ron Osman Omar, amesema kuinuka kwa uhusiano kati ya China na Afrika hadi kufikia ushirikiano wa hali zote, kunaakisi si kama tu kuaminiana kisiasa, bali pia kuongezeka kwa ushirikiano wa kiuchumi na kimaendeleo, kukichukua nafasi muhimu katika kuendeleza maslahi ya Dunia ya Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha