Lugha Nyingine
Safari ya mchoro wa Tinganga: Kutoka Tanzania hadi pwani za ushairi za Gulangyu, China
Kisiwa cha Gulangyu, "Bustani ya Baharini" ya kuvutia karibu na pwani ya Xiamen, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, kwa muda mrefu kimekuwa mahali pa kukutana tamaduni, ambako historia, muziki na maisha ya kila siku huchangamana katika mazingira ya kipekee ya ushairi.
Hivi karibuni, Aris, kutoka Tanzania, alisafiri akiwa na picha ya Tingatinga kutoka nchi yake kwenda katika kisiwa hicho na kuanza safari ya kipekee ya biashara ya kubadilishana vitu kwa vitu na mabadilishano kwenye kisiwa hicho.
Michoro hiyo ya picha ya Tingatinga yenye asili ya Tanzania, inajulikana kwa rangi zake angavu, uoneshaji wa mazingira ya asili na wanyamapori, na mtindo wa sanaa ya jadi wenye hali motomoto, na inachukuliwa kuwa moja ya aina za sanaa maarufu zaidi za Afrika Mashariki.
Kwa kutumia mchoro kama mahali pa kuanzia kwa ajili ya mabadilishano, Aris alipokea mfululizo wa vitu ambavyo kila kimoja kilifichua upande tofauti wa kisiwa hicho cha Gulangyu. Kadi ya posta inayoonyesha mandhari za kifahari za usanifu wa kimataifa wa Gulangyu, akizungumzia kwenye urithi huo wa karne wa kuwa makazi ya Wachina wa ng'ambo; karatasi yenye ala za muziki zinazovumisha sifa yake ya kuwa "Kisiwa cha Piano"; Kikaragosi cha jadi kinachoangazia mvuto wa urithi wa utamaduni usioshikika wa kusini mwa Fujian; pai ya kienyeji inayobeba ukarimu wa mila za upishi za kisiwa hicho; na juzuu ya mashairi yanayokamata moyo wa fasihi na kimapenzi ambao umekuwa ukiielezea Gulangyu kwa muda mrefu.
Kupitia mabadilishano haya, kisiwa hicho kimejifungua si tu kama kivutio cha watalii, bali kama mandhari hai ya kitamaduni iliyoumbwa na historia, sanaa na muunganisho wa binadamu.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma