Lugha Nyingine
China yatunuku nishani ya heshima ya juu zaidi ya vijana kwa watu 29 na mashirika 30

Vijana waliotunukiwa wa Nishani ya Vijana ya Mei Nne ya China 2026 wakipiga picha pamoja kwenye hafla ya kutoa nishani iliyofanyika Beijing, mji mkuu wa China, Aprili 27, 2026. (Xinhua/Cai Yang)
BEIJING - Ofisi husika za China zimeamua kuwatunuku vijana 29 na mashirika 30 nishani ya heshima ya juu zaidi ya vijana kwa kusifu kazi yao ya kupigiwa mfano.
Kamati Kuu ya Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China na Shirikisho Kuu la Vijana la China wametangaza uamuzi huo wa kutoa Nishani ya Vijana ya Mei Nne ya China 2026 katika taarifa yao iliyotolewa jana Jumatatu.
Watunukiwa wa nishani hiyo ni wa kutoka sekta mbalimbali wakiwemo pamoja na mtaalamu wa matibabu ya magonjwa magumu, mtaalamu wa teknolojia ya usafiri kwenye anga, ofisa wa mambo ya chama ya mashinani, ofisa wa usimamizi wa mipaka na mtafiti wa fizikia.
Mashirika yaliyopewa tuzo ni pamoja na shirika moja la Shanghai la kulea na kukuza mfano mkubwa wa AI, timu ya usafirishaji wa bidhaa wa reli na timu inayojikita katika utafiti wa ncha za dunia.

Wajumbe wa mashirika yaliyopewa Nishani ya Vijana ya Mei Nne ya China 2026 wakipiga picha kwenye hafla ya kutoa nishani iliyofanyika Beijing, Aprili 27, 2026. (Xinhua/Cai Yang)

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma