Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (katikati, mbele) akizungumza kwenye mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya usalama na ulinzi wa njia za maji katika eneo la bahari, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Aprili 27, 2026. (Xinhua/Xie E)
UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jana Jumatatu kwenye mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama juu ya usalama na ulinzi wa njia za maji katika eneo la baharini ametoa wito wa kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.
"Haki na uhuru wa usafirishaji kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz lazima viheshimiwe ... Kanuni hizi lazima zidumishwe kikamilifu, na bila kuchelewa," amesema.
"Ninatoa wito kwa pande zote: fungueni mlango huo, acheni meli zipite, bila ya tozo, bila ya ubaguzi, acheni biashara irejee, acheni uchumi duniani upumue," amesema Guterres
Amesema tangu mapema Machi, mvurugiko wa usafirishaji kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz umeathiri usalama wa nishati, usambazaji wa chakula na biashara duniani.
Mlango-Bahari wa Hormuz ni moja ya maeneo muhimu zaidi ya baharini duniani. Unabeba takriban sehemu ya moja ya tano ya biashara ya mafuta duniani, moja ya tano ya gesi asilia ya kimimika duniani, na karibu theluthi moja ya mbolea zinazouzwa kimataifa. Upitaji salama na usiozuiliwa ni hitaji la kiuchumi na kibinadamu, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema.
"Mvurugiko wa usafirishaji kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz umeleta mshtuko wa ghafla wa kiuchumi, na kila mmoja analipa gharama: hali yenye utete mkubwa katika masoko ya nishati na bidhaa, kuongezeka kwa gharama za usafiri na bima, na mvurugiko mbaya zaidi wa mnyororo wa usambazaji tangu COVID-19 na mgogoro wa Ukraine," amesema Guterres.
Guterres amesema wakati huu unahitaji kujizuia, mazungumzo na ujengaji imani. Ametoa ofa ya ofisi zake nzuri kusaidia kupata msingi wa pamoja.
Kwa upana zaidi, ametoa wito wa kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa, juhudi za kushughulikia vyanzo sababishi vya ukosefu wa usalama baharini, na kuzidisha mazungumzo na ushirikiano.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mjadala wa wazi juu ya usalama na ulinzi wa njia za maji katika eneo la bahari, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Aprili 27, 2026. (Xinhua/Xie E)

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma